Benki kuu ya tanzania yazitoza faini benki tano za biashara kwa kukiuka kanuni za kuzuia utakatishwaji wa fedha

Benki
Kuu ya Tanzania imezitoza faini benki tano za biashara kwa kukiuka
kanuni namba 17, 22 na 28 za Kanuni za Kuzuia Utakatishwaji wa Fedha
Haramu za mwaka 2012 kwa kushindwa kuhakiki taarifa za utambulisho wa
wateja na kushindwa kuwasilisha taarifa ya miamala yenye kuleta mashaka
katika Kitengo cha Kuzuia Fedha Haramu (FIU). Benki hizo na kiasi cha
faini ni kama ifuatavyo:


1.African Banking Corporation (T) Limited TSH 145 milioni 2. Equity Bank (Tanzania) Limited TSH 580 milioni 
3. I&M Bank (T) Limited TSH 655 milioni 
4. UBL Bank (T) Limited TSH 325 milioni 
5. Habib African Bank Limited TSH 175 milioni

Pamoja na faini hizo, Benki Kuu ya Tanzania imezitaka benki hizo
kutekeleza yafuatayo ndani ya kipindi cha miezi mitatu toka tarehe faini
zilipotozwa:

 1. Kupitia
  upya taarifa za wateja wao na kuhakikisha kwamba zinakidhi matakwa ya
  kisheria na kanuni zilizopo za uhakiki wa utambulisho wa wateja (KYC);
 2. Kuwasilisha taarifa ya miamala yenye kuleta mashaka ambayo ilitakiwa kuwasilishwa FIU;
 3. Kufanya
  tathmini ya ubora wa mifumo ya ndani ya kibenki na kuchukua hatua
  stahiki kuhakikisha kuwa mifumo hiyo ipo madhubuti kwa lengo la kukinga
  mapungufu hayo hayarudii tena; na
 4. Kuwachukulia
  hatua stahili za kinidhamu, wafanyakazi wote waliohusika kufanikisha
  ufunguaji wa akaunti za amana kinyume na kanuni za kumtambua mteja
  (KYC).

Benki
Kuu ya Tanzania inapenda kuzikumbusha benki na taasisi za fedha
kuhakikisha kuwa zinafuata sheria na kanuni zilizopo nyakati zote. 


BENKI KUU YA TANZANIA 
botcommunications@bot.go.tz 
19 SEPTEMBA 2019

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *