Benki ya tpb yatoa elimu kwa walimu wastaafu wilayani kahama

Benki ya TPB  imetoa elimu kwa walimu wastaafu wilayani kahama kuhusu
maboresho ya huduma zao lakini namna gani mzee anapaswa kuwekeza na kuwa
na matumizi bora ya pesheni yake.
Akizungumza katika mkutano huo Januari 4,2020  Meneja wa Benki ya TPB mkoa wa Shinyanga Jumanne Wagana
aliwapa wazee Elimu  ya BIMA ya Maisha ya Tsh 1000/=, Biashara ya
akaunti ya Amana kwa muda maalumu inayokupa faida mpaka 12%,  jinsi ya
kupata mitaji kupitia mikopo ya riba nafuu ya wastaafu, mikopo ya
kilimo, mikopo ya biashara n.k.
 Katika mkutano huo ambao ulifadhiliwa na Benki ya TPB wastaafu
mbalimbali walitoa shukrani zao za dhati kwa Benki ya Serikali ya TPB
kwa kuwajali na kuwawezesha wafikie malengo yao ambayo walikuwa
hawajakamilisha wakati wanastaafu. 
Naye Kaimu Meneja wa tawi la Kahama  Patrice Garani  akichangia amewaomba wazee wasiogope kukopa kwani mikopo ya TPB ina Bima.
Meneja wa TPB Mkoa wa Shinyanga Ndg Jumanne Wagana akitoa Elimu kwa Waalimu Wastaafu wilayani ya Kahama.
Walimu Wastaafu wakifuatilia kwa umakini Wawezeshaji kutoka Benki ya TPB wakitoa elimu ya fedha, mikopo na ujasiriamali.