Bidhaa zilizoisha muda wa matumizi,zilizobadilishwa lebo zakamatwa kwenye maduka shinyanga mjini

Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa
Shinyanga ikishirikiana na wakaguzi kutoka Shirika la Viwango Tanzania
TBS imefanikiwa kukamata bidhaa zilizoisha muda wa zikiendelea kuuzwa
katika maduka makubwa maarufu kama Supermarket mjini Shinyanga hali
ambayo ni hatari kwa afya za watumiaji wa bidhaa hizo.


Bidhaa hizo zimekamatwa jana kutokana na msako katika maduka mbalimbali
Mjini Shinyanga na kukamata shehena ya bidhaa mbalimbali ikiwemo
chakula na vipodozi ambazo zimeisha muda wa kutumika vikiendelea kuuzwa
madukani.
Akizungumza baada ya kufanya ukaguzi huo,Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya
Ulinzi na Usalama ya mkoa Mhe. Jasinta Mboneko ambaye ni Mkuu wa wilaya
ya Shinyanga amesema licha bidhaa nyingi madukani kuwa zimeisha muda wa
kutumika pia wamebaini kuna udanganyifu mkubwa wa kubadilisha lebo za
muda wa matumizi katika bidhaa mbalimbali ili ziendelee kuuzwa sokoni.
Naye Mkaguzi wa kutoka Shirika la Viwango Tanzania TBS Helen Andrew amesema operesheni hiyo sasa ni endelevu kwa mikoa yote.
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa Mhe. Jasinta Mboneko akiangalia bidhaa ndani ya duka