Bonanza la kataa ukatili smaujata mkoa wa shinyanga wazungumza na jamii

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mwenyekiti wa kampeni ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi
wa Jamii Tanzania SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bi. Nabila Kisendi ameikumbusha
jamii kutoa taarifa za ukatili ikiwemo ubakaji, ulawiti pamoja na ndoa za
utotoni.

Ameyasema hayo akiwa mgeni rasmi katika bonanza la
kupinga ukatili Cheupe Cup ambao limefanyika kwa siku sita mtaa wa Dome kata ya Ndembezi
Manispaa ya Shinyanga na kwamba bonanza hilo limekwenda sanjari na michezo
mbalimbali katika uwanja wa Balina English Medium primary school.

Madam Kisendi pamoja na mambo mengine ameisihi jamii
kupaza sauti juu ya ukatili kwa kutoa taarifa za vitendo hivyo ili hatua zaidi
ziweze kuchukulia na serikali.

Amewasisitiza watoto kutoa taarifa za ukatili
unaofanyika shuleni huku akiwaomba wazazi na walezi kujenga tabia ya kuzungumza
na watoto baada ya kutoa shule ikiwa ni pamoja na kuwakagua kwa lengo la
kuimarisha usalama wao.

“Pamoja
na kwamba mtaa wa Dome uko vizuri kiutendaji lakini upo ukatili unaoendelea
kufanya katika eneo hili, sasa hivi kuna janga kubwa linaendelea katika Mkoa
wetu wa Shinyanga ukatili wa kimwili hasa watoto kubakwa na wengine kulawitiwa na
haya yote uzembe unaanzia kwenye familia zetu wazazi kaeni vizuri na watoto
wenu msiwatelekeze hakikisheni wanapata haki zao sasa hivi watoto kesho wanafungua
shule kwanza mtoto usikubali kushikwa shikwa au kupewa zawadi na mtu
usiyemfahamu mwisho wake atakukatili”.
amesema Mwenyekiti Madam
Kisendi

“Sisi
SMAUJATA tupo kwa ajili ya kuibua ukatili unaofanyika kwahiyo mtu yoyote na
wewe mtoto ukifanyiwa ukatili toa taarifa usikae kimya akiwa mama na baba zetu
kuna vitu vibaya vinafanyika huko kwenye jamii paza sauti tupeni taarifa sisi
tutawatetea kumbuka ukatili unarudisha nyuma maendeleo upo ukatili wa kimgono
unafanyika, ukatili wa kiuchumi lakini pia zipo mimba za utotoni madhara yake
ni makubwa husababisha vifo kuwa makini epuka kufanyiwa ukatili epuka kufanya
ukatili”.amesema Madam Kisendi

“Akina
mama tuwe walezi wa watoto wetu hakikisha mtoto yoko salama anapocheza,
anapotoka shule mkague  niwaombe sisi
sote tuliohudhuria hapa tukawe mabalozi wazuri kwa wengine mkawaambie watoe
taarifa za ukatili SMAUJATA tutazipokea na kuzifikisha sehemu husika”.
amesema
Madam Kisendi

Kwa upande Afisa ustawi
wa jamii Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga Bwana Leopald Hamza
ameeleza
hatua mbalimbali za kufanya baada ya kubaini vitendo vya ukatili katika jamii.

“wengi
wanapokumbana na masuala ya ukatili hawajui nini cha kufanya wengi wamekuwa
wakiondoa ushahidi unakuta mtoto amebakwa au amelawitiwa mzazi hajui nini cha
kufanya anamuogesha au anambadilishia nguo mtoto unapokutana na mtoto kafanyiwa
tukio hilo usibadilishe kitu chochote wala usimuogeshe kitu cha kwanza nenda
kwa mtendaji wako au mwenyekiti au dawati la polisi au kwa afisa ustawi wa
jamii au ripoti kwa hawa SMAUJATA ili uweze kupata msaada wa haraka na sisi
tutakuunganisha na madakitari kwa uchunguzi zaidi ukiwa na vielelezo vya
ushahidi ambavyo vitatusaidia sisi kuweze kushinda kesi”.
amesema
Afisa ustawi Hamza

Viongozi mbalimbali wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga
wametoa elimu ya ukatili huko baada ya wananchi waliohudhuria bonanza hilo
wakiipongeza kampeni ya SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga kwa kutoa elimu hiyo ambapo
wameahidi kuendelea kutoa taarifa za ukatili unaoendelea kufanyika katika
jamii.

 

Mgeni rasmi Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bi.
Nabila Kisendi na viongozi mbalimbali wakiwa katika zoezi la kukagua timu za
mpira leo Jumapili Julai 2,2023 katika uwanja wa Balina English Medium primary
school mtaa wa Dome kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.