Brela kutoa huduma za urasimishaji wa biashara kwenye fursa jijini dodoma

Kaimu Mkurungezi Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA)  Emanuel Kakwezi akizungumza


WAKALA
wa Usaji wa Biashara na Leseni nchini (BRELA) unatarajiwa kutoa huduma
za urasimishaji wa biashara Octoba 18 na Octoba 19 Jijiji Dodoma  kwenye
ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma wakati wa fursa 2019.



Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mkurungezi Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela)  Emanuel
Kakwezi  ambaye pia alifanya  ukaribisho kwa wana Dodoma alisema
watatoa huduma mbalimbali wakati wa fursa 2019 huku wakiwataka wakazi wa
mkoa huo kuchangamkia fursa hiyo muhimu.

Alisema kwamba huduma ambazo zitatolewa wakati wa Fursa Dodoma ni usajili wa Majina ya Biashara, Kampuni, Nembo za Biashara na huduma, Hataza, Leseni Daraja A, Leseni za Viwanda.


Kaimu Mkurungezi Mkuu alisema wameamua kishiriki kwenye Fursa  mwaka huu kutokana uhitaji wa wananchi juu ya ujarasimishaji Biashara zao  Pia wameamua kushiriki kutokana na kauli mbiu ya mwaka huu inayosema “Leta  Solution” ikiwa kama Taasisi ya Brela ni moja ya solution kwenye Biashara  na ubunifu wa wasajiriamali ili kuendana na Serikali ya viwanda ya sasa.

Kikubwa zaidi kilichofanya kushiriki ni kuwafikia wananchi kwa ukaribu zaidi na kuwahudumia kwa ukaribu zaidi.

Kakwezi alisema Brela pia Itashiriki kwenye Fursa mikoa yote ambayo  imebaki baada ya Dodoma na watakuwa wanatoa huduma zote zinazotolewa na  Brela, ambapo mikoa hiyo ni Tanga, Arusha na Dar es Salaam. 

Hata hivyo alitoa  rai kwa wananchi wote kutumia fursa hii  ili kuweza kupata huduma za Brela  kwani kutakuwa na team ya Brela ambayo  itatowa huduma zote na wananchi watakao kidhi masharti kama ya kuwa na  Namba ya Kitambulisho cha NIDA na vingezo vingine wataweza kuondoka na  vyeti vya Usajili.