Brela yapongezwa na kamati ya bunge ya kudumu ya viwanda, biashara na mazingira kwa kuboresha utendaji kazi

 

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Makampuni na
majina ya biashara ndugu, Meinrad T. Rweyemamu akiwasilisha taarifa ya
namna ya usajili wa makampuni unavyofanywa na Wakala ya Usajili wa
Biashara na Leseni (BRELA) kwa Kamati ya kudumu ya bunge Viwanda,
Biashara na Mazingira, iliyofanyika leo Juni 9,2021 Bungeni jijini
Dodoma.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya
Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Ndugu Godfrey Nyaisa akitoa
ufafanuzi wa baadhi ya masuala yaliyoulizwa na wabunge wa kamati ya
kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira katika kikao
kilichofanyika leo Juni 9 2021 Bungeni jijini Dodoma.

Msajili msaidizi Mkuu miliki ubunifu
kutoka BRELA Bi. Loy Mhando akitoa ufafanuzi katika kikao cha kamati ya
kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira katika kikao
kilichofanyika leo Juni 9, 2021 Bungeni jijini Dodoma.

Kaimu Mkuu wa sehemu ya Leseni za
Biashara akitoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja za waheshimiwa wabunge
katika kikao cha kamati ya kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara na
Mazingira katika kikao kilichofanyika leo Juni 9,2021 Bungeni jijini
Dodoma.

Mwenyekiti wa kamati ya bunge Viwanda,
Biashara na Mazingira Mhe. David Kihenzile (Mb) akizungumza wakati wa
kikao cha kamati ya kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira
kupokea taaraifa ya utendaji wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni
(BRELA) katika kikao kilichofanyika leo Juni 9, 2021 Bungeni jijini
Dodoma.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.
Prof. Kitila Mkumbo (Mb) akitoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja
zilizojadiliwa katika kikao cha kamati ya kudumu ya Bunge Viwanda,
Biashara na Mazingira kupokea taaraifa ya utendaji wa Wakala ya Usajili
wa Biashara na Leseni (BRELA) kilichofanyika leo Juni 9, 2021 Bungeni
jijini Dodoma.

Mbunge wa Jimbo la Bunda Vijijini
Peter Mwita Getere, akichangia katika kikao cha kamati ya kudumu ya
bunge Viwanda, Biashara na Mazingira kilichofanyika leo Juni 9, 2021
Bungeni jijini Dodoma.

Mbunge wa Jimbo la Buchosa Mhe.Eric
Shigongo ,akichangia katika kikao cha kamati ya kudumu ya bunge Viwanda,
Biashara na Mazingira kilichofanyika leo Juni 9, 2021 Bungeni jijini
Dodoma.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.
Prof Kitila Mkumbo amesema kuwa Serikali itaendelea kuiwezesha BRELA
kuboresha utoaji wa huduma zake kwa wafanyabiashara kwa kuwa ni chombo
muhimu katika ukuaji wa Sekta ya Biashara nchini.

Waziri Mkumbo ameyasema hayo wakati wa
semina iliyolenga kuwaelimisha wajumbe wa Kamati hiyo kuhusu
utekelezaji wa majukumu ya BRELA na mafanikio yake iliyofanyika leo Juni
9,2021 katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.

Nayo, Kamati hiyo imeipongeza BRELA
kwa kuboresha utendaji kazi na kuitaka iendelee kuongeza ubunifu katika
kuboresha huduma na kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma hizo hadi
vijijini.

Aidha, Wajumbe wa Kamati hiyo wametoa
maoni na mapendekezo mbalimbali yanayolenga kuboresha huduma na
bidhaa zinazotolewa na BRELA ikiwemo Uhuishaji wa taarifa, uhusiano wa
biashara kati ya Tanzania Bara na Zanzibar, Umiliki Manufaa na Sera ya
Taifa ya Umiliki Binafsi

Akiwaelimisha Wajumbe wa Kamati hiyo,
Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Bw. Godfrey Nyaisa alisema BRELA inaendelea
kuboresha utoaji wa huduma zake kwa njia ya mtandao kwa kutumia mifumo
mbalimbali ya Sajili kwa lengo la kuboresha mazingira ya biashara
nchini.

Bw.Nyaisa pia amesema kuwa BRELA
inaendelea kushirikiana na Mamlaka za Serikali za Mtaa na SIDO katika
utoaji wa huduma, na imeingia makubaliano mbalimbali ya Kikanda na
Kimataifa katika nyanja za umiliki wa ubunifu.

Amesema kuwa jukumu la msingi la
BRELA ni kusimamia ufanyikaji wa Biashara nchini kwa kuzingatia sheria
na kanuni za biashara zilizopo.

Afisa huyo amesema ili kuhakikisha
kuwa mazingira ya uwekezaji, uanzishaji na urasimishaji biashara nchini
yanakuwa wezeshi, BRELA imeandaa Mpango Mkakati wa saba unaoanza
kutekelezwa mwaka 2021/22 na unalenga kuboresha utoaji wa huduma za
sajili na leseni ili kuwa na ukuaji endelevu wa viwanda na maendeleo ya
uchumi.

Hata hivyo amesema kuwa mpango huo
umelenga kufanya maboresho ya sheria zinazosimamiwa na BRELA ili
kuendana na mahitaji ya kibiashara ya sasa na mipango ya kitaifa.

Ametaja mambo yaliyotekelezwa hadi
sasa katika mpango mkakati wa sita, Bwana Nyaisa alisema kuweka mifumo
ya Kielektroniki ya Utoaji wa Huduma za Sajili (ORS) na Utoaji wa Leseni
za Biashara (NBP).

Pia ametaja utengenezaji na uboreshaji
wa mifumo ya utendaji kazi kama Mfumo wa ki-elektoniki wa Majalada –
“e-Office”, Matumizi ya Mfumo wa Ulipaji Serikalini (MUSE), na Mfumo wa
ki-elekroniki wa mahudhurio (e- Attendance System).

Bw.Nyaisa amesema pia uandaaji wa
nyaraka mbalimbali za Kiutendaji na Kiutawala kama Mpango Mkakati –
Strategic Plan 2021/22– 2025/26, Mkakati wa Mawasiliano na Huduma kwa
Mteja (Communication and Customer Service Strategy), Kanuni za
Utumishi, Fedha, na maendeleo ya Watumishi.