Buriani mwanahabari lobulu, *historia fupi ya marehemu william nicholaus lobulu*

Anaandika Suckdev Chatbar
Marehemu William Lobulu enzi za uhai wake


Mzee William Lobulu alizaliwa 20 Desemba 1951 Sanawari, Arusha.

Alifanya
kazi Shirika la Habari Tanzania (SHIHATA) baada ya kuhitimu Shahada ya
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadaye alipata Shahada ya Uzamivu Chuo
Kikuu cha Meriland, Marekani alipokuwa  Mkufunzi katika Chuo cha
Uandishi wa Habari Tanzania, (TSJ).


Alifanya kazi za uandishi wa habari, uhariri pamoja na kuchapisha gazeti la “Arusha Times”.

Pia
alifanya kazi ya ushauri yaani “consultancy” inayohusiana na masuala ya
machapisho katika mashirika ya mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.

Marehemu
alibatizwa kanisa la KKKT Ilboru. Alifunga ndoa ambayo ilibarikiwa
Kanisa la KKKT Mjini Kati mwaka 1986. Mzee William ameacha mke na watoto
watatu na mjukuu mmoja. 

Alikuwa
akisumbuliwa na asthma ambayo ilimshika ghafla na taa yake ikazima
alipoitwa mbinguni saa 12 asubuhi Jumapili tarehe 6 Oktoba 2019.

Familia inatoa shukrani kwa wote waliohusika kumhudumia marehemu kwa hali na mali kuhusiana na afya yake.

Tunashukuru Wachungaji, Wainjilisti na Wazee wa Kanisa na watumishi wote waliokuwa wakimpa huduma mbalimbali za kiroho.

Marehemu atakumbukwa kwa ushirikiano, upole, ucheshi na moyo wa huruma kwa watoto na watu wote kwa ujumla. 

BWANA ametoa, BWANA ametwa jina la BWANA lihimidiwe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *