Ccm nao kutoa tamko kesho kutwa kuhusu uchaguzi serikali za mitaa

Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole
amesema chama hicho kwa sasa kinaendelea kufuatilia muenendo wa zoezi
zima la uchaguzi wa Serikali za Mitaa, na kinatarajia kutoa tamko lake
Novemba 13, 2019.

Polepole
ametoa kauli hiyo Leo Novemba 11, 2019 kupitia ukurasa wake wa Twitter,
huku zoezi zima la uchaguzi huo likiwa limekumbwa na changamoto kadhaa
ikiwemo wagombea wengi wa vyama mbalimbali kuenguliwa.

Kutokana
na changamoto hizo, jana Waziri wa Nchi ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe.
Selemani Jafo alitengua maamuzi yote na kuamua kuwaruhusu wagombea wote
nchini waliochukua fomu na kuzirejesha kushiriki uchaguzi wa Serikali za
Mitaa bila kujali kama walienguliwa isipokuwa kwa wale wasio raia wa
Tanzania, hawakujiandikisha au wamejiandikisha mara mbili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *