Ccm yawaonya walioanza kampeni za urais na ubunge kabla ya wakati

Katibu
Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally amewaonya wanachama wa chama hicho
tawala walioanza mikakati ya kutaka kupitishwa kuwania udiwani, ubunge
na urais akibainisha kuwa kufanya hivyo ni makosa.



“Watu
wa namna hiyo(walioanza mapema mikakati ya kutaka kupitishwa kuwania
udiwani, ubunge na urais) hawatavumiliwa kwa kuwa taratibu za kuwania
uongozi, nafasi mbalimbali katika chama hicho zipo wazi na zina muda
wake” Dk. Bashiru Ally, Katibu mkuu wa CCM

Ametoa
kauli hiyo leo Jumanne Desemba 3, 2019 katika ziara yake kisiwani
Pemba, Zanzibar wakati akizungumza na kamati ya siasa Wilaya ya
Chakechake.