Chadema mbeya wapongeza harakati za naibu spika dr. tulia ackson


Naibu Spika Dr. Tulia Ackon kwa
kushirikiana na taasisi yake ya Tulia Trust amefanya ziara katika Shule
ya Sekondari Ivumwe iliyopo mkoani Mbeya ambapo ametoa msaada wa
Shilingi Milion mbili na laki tano (Tsh. 2,500,000/-) aliyokuwa ameahidi
katika shule hiyo ili kusaidia uboreshaji wa miundombinu katika shule
hiyo ikiwemo uchakavu wa madarasa, maabara pamoja na bweni la watoto wa
kike.
Aidha, Dr. Tulia amesisitiza
kwamba kupitia taasisi hiyo ya Tulia Trust ambayo inajikita katika
kusaidia sekta mbalimbali nchini ikiwemo Elimu na Afya ataendelea kutoa
misaada mbalimbali katika Shule ikiwa ni sehemu ya kushiriki kuunga
mkono jitihada za Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli.
Akizungumza na Wanafunzi wa Shule
hiyo Dr. Tulia amesema “Mimi nimetembelea shule nyingi sana hapa nchini,
watoto wa shule hii ya Ivumwe mazingira yenu ni mazuri mno
ukilinganisha na shule nyingine, kwamaana hiyo hakuna sababu yoyote ya
kufeli, natamani sana kuzisikia hadhithi nzuri za ufaulu. Niwaombe sana
watoto wazuri msome kwa bidii ili muweze kulisaidia taifa, hata mimi
hapa mnaponiona na huu Udaktari wangu sio kanakwamba nimepewa tu,
hapana, ni Udaktari wa kisomo hivyo na nyie mkazane kusoma ili kutimiza
ndoto zenu”-Dr. Tulia
Katika hafla ya kukabishi fedha
hizo Diwani wa Kata ya Mwakibete Lucas Mwampiki (CHADEMA) amesema
maendeleo hayana itikadi hivyo anampongeza Dr. Tulia kwa kuchangia
maendeleo katika Kata yake kwani ni mara ya tatu sasa Naibu Spika
anachangia shughuli za maendeleo katika Kata hiyo. “Nakushukuru Naibu
Spika kwa shughuli unazozifanya kwani katika shule hii inayosimamiwa na
CCM mimi nina ndugu zangu 52 wanaosoma hapa na sifa inayopatikana ni ya
Mwakibete na Mbeya kwa ujumla” alisema Mwampiki

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *