Daktari feki anayetajwa kusababisha vifo vya wagonjwa atupwa jela kigoma

Picha ya mfano wa daktari
Mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Kigoma imemhukumu kwenda jela miaka
miwili na nusu daktari feki ambaye anatajwa kusababisha vifo vya
wagonjwa kupitia kazi ya udaktari ikiwemo kufanya upasuaji.
Daktari huyo feki aitwaye Maxmillian Martin amepelekwa mahakamani hapo
kwa makosa matano likiwemo la kufoji cheti cha shahada ya kwanza ya
udaktari kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam, cheti cha mafunzo kwa
vitendo cha hospitali ya rufaa ya Muhimbili, cheti cha chama cha
madaktari, kufanya kazi ya udaktari wakati si daktari na kufanya kazi ya
udaktari bila leseni.
Inaelezwa alifanya kazi katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu na
kulipwa mshahara wa zaidi ya milioni mbili kwa zaidi ya miaka miwili na
miongoni mwa mashahidi ambaye alitoa taarifa polisi alieleza alichukua
hatua hiyo baada ya kuona vifo vikiongezeka kwa anao wahudumia.
Akisoma mwenendo wa kesi hiyo hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya
wilaya ya Kigoma Keneth Mutembei amesema, mshtakiwa alikana kuwa vyeti
hivyo ni vyake ila alikuwa anafanya kazi kwa kujitolea ili apate ada ya
kwenda chuo kwani alishindwa kuendelea na masomo ya udaktari mwaka 2004
na kuwa yeye ni kijana mwenye akili na matokeo ya daraja la nne.
Alipoambiwa kujitetea kabla ya hukumu aliiomba mahakama hiyo kumpa
kifungo cha nje kutokana na kutegemewa na familia na watoto wanne na
kuwa afya yake si njema hivyo hakimu kuamua mshtakiwa kwenda jela kwa
miaka miwili na nusu.
Chanzo – EATV

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *