Darasa laanguka na kuua wanafunzi 7 shuleya precious talent




Wanafunzi
saba wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa baada ya jengo la darasa la
Shule ya Precious Talent kuanguka eneo la Ngado Nairobi nchini Kenya
saa 1 asubuhi leo Jumatatu Septemba 23, 2019. 





Shule hiyo ipo mkabala na Barabara ya Ngong’; shughuli za uokozi
zinaendelea kwa sasa huku ikiarifiwa tayari wanafunzi zaidi ya 50
wametolewa kwenye vifusi na kupelekwa Hospitali Kuu ya Kitaifa ya
Kenyatta (KNH). 



Kwa Mujibu wa Shirika la Msalaba Mwekundu Kenya shughuli ya uokoaji
inaendelea na wanafunzi wanne wamepelekwa Hospitali ya Taifa ya
Kenyatta.



Kamanda wa polisi George Seda na mbunge wa eneo la Dagoreti, John
Kiarie, wamethibitisha kuongezeka kwa idadi ya vifo kutokana na ajali
hiyo.



Mkurungezi wa shule hiyo ya kibinafsi, Moses Wainaina Ndirangu,
amaeiambia Runinga ya Citizen nchini Kenya kuwa jengo hilo liliathiriwa
na ujenzi wa bomba la maji taka karibu unaoendelea karibu na hapo.




Baadhi ya wanafunzi wanasemekana kukiimbilia makaazi ya watu walio
karibu na mtaa waDagoretti, Magharibi mwa Jiji la Nairobi baada ya jengo
la shule kuporomoka.