Dawasa kuchangia matofali 2000 ujenzi wa ofisi ya uwamakizi muheza

 


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Dawasa Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange akizungumza mara baada ya kutembelea ofisi ya Uwamakizi wilayani Muheza wakati wa ziara yao ya siku moja kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo na kulia ni
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja

Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo akizungumza wakati wa ziara hiyo kushoto ni
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa
Mazingira Jijini Dar es Salaam (Dawasa)
Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange


Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly akizungumza jambo wakati wa ziara hiyo

Mkurugenzi
wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly katikati akisisitiza jambo kwa
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa
Mazingira Jijini Dar es Salaam (Dawasa) Jenerali Mstaafu Davis
Mwamunyange kushoto wakati wa ziara hiyo kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu
wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja wa kwanza kushoto ni  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa
Mazingira Jijini Dar es Salaam (Dawasa) Jenerali Mstaafu Davis
Mwamunyange kushoto akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu
wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja kulia wakati wa ziara hiyo
Mwenyekiti
wa Kikundi cha Uwamakizi wilayani Muheza Twaha Rajabu kushoto akieleza
namna wanavyotunza mazingira katika vyanzo vya maji kwa wajumbe wa bodi
ya wakurugenzi ya Dawasa wa pili kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Dar es
Salaam (Dawasa) Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange
Mwenyekiti
wa Kikundi cha Uwamakizi wilayani Muheza Twaha Rajabu kushoto akieleza jambo kwa wajumbe wa bodi
ya wakurugenzi ya Dawasa kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Dar es
Salaam (Dawasa) Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange

MAMLAKA
ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Dar es Salaam (Dawasa) imeahidi kutoa
matofali 2000 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa ofisi ya umoja
wa wakulima wahifadhi wa Mazingira
Kihuwi (Uwamakizi) iliyopo Kijiji cha Kimbo Kata Potwe Tarafa ya Amani wilayani
Muheza Mkoani Tanga.

Ahadi
hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Dawasa Jenerali Mstaafu
Davis Mwamunyange wakati wa ziara yao ya kimafunzo ya siku moja wilayani Muheza
ambapo walielezwa jitihada za umoja huo kuanza ujenzi wa ofisi yao kwa nguvu
zao.

 Ziara hiyo iliandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi
na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) ambapo walitembela maeneo mbalimbali ikiwemo
eneo la Bustani ya Uwamakizi katika mlima wa mfano wa shughuli za uwamalikizi.

Alisema wamefika
kwenye umoja huo na kusikia jitihada za kuanzisha ujenzi wa ofisi yao kwa nguvu
zao wenyewe licha ya jitihada wanazofanya kwenye vyanzo vya maji na wameweza
kufyetua matofali 3000.

“Lakini ili nasi
tusiondoke hapa bila kuacha kumbukumbu yoyote tumeamua kuchangia juhudi hizo
kwa kutoa matofali 2000 kuunga mkono ujenzi wa ofisi hiyo“Alisema Jenerali
Mstaafu Mwamunyange.

 Awali akizungumza
wakati wa ziara hiyo Mwenyekiti wa Uwamakizi Twaha Mbaruku alisema kwamba wana
ujenzi wa ofisi na kwa sasa wamekwisha kupata tofali 3200 kwa lengo la kuanza
ujenzi.

“Mmekuja hapa
tumeshindwa kuwaingiza ofisini tulipokodi kwenye jengo dogo la Serikali kwa
sababu ugeni huu hauwezi kuingia lakini tumejiongeza kuona vema tujenge ofisi
kubwa”Alisema

Akielezea kuhusu
umoja huo Mwenyekiti huyo alisema uwamakizi wataendelea kupambana kuhakikisha
vyanzo vya maji vinahifadhiwa na kutunzwa ili viweze kuwa endelevu.

 Alisema wao wanachangamoto ndogo lakini wanashukuru
Tanga Uwasa tokea walipoanzisha mradi huo 2013 hawakurudi nyuma waliendelea
kuongeza mapambano nao na ushirikiano na makubaliano yaliendelea