Dc chongolo ataka usawa kwa watu wenye ulemavu, asema wasinyanyapaliwe.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.
Daniel Chongolo akizungumza na wajumbe wa kamati ya watu wenye ulemavu ,
kushoto ni Afisa utumishi wa halmashauri Faudhia Nombo.


Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni , Mhe.
Daniel Chongolo akiwa katika hafla ya uzinduzi wa kamati ya watu
wenyeulemavu wa halmashauri , wa kwanza kushoto ni Afisa utumishi
Faudhia Nombo, aliyesimama kulia ni Judithi Kimaro , Afisa ustawi wa
jamii ambaye ni katibu wa kamati hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo ameiasa jamii kutojihusisha na tabia ya
kuwanyanyapaa watu wenyeulemavu kwakuwa nawao wanahaki ya kupata
hakizote kama ilivyo kwa watu wengine.
Mhe. Chongolo
ametoa kauli hiyo leo katika halmashauri ya Kinondoni wakati wa uzinduzi
wa kamati ya watu wenye ulemavu ambapo pamoja na mambo mengine amesema
ipo dhana iliyojengeka ya kuwanyanya paa watu hao na hivyo kueleza kuwa
kufanya hivyo ni makosa na kusisitiza kuwa nilazima itendeke haki na
usawa.
Amesisitiza kuwa
watu wenye ulemavu wanahaki ya kupewa nafasi mbalimbali na kusema kuwa
wote wenye dhamana ya uongozi katika halmashauri hiyo ni lazima
kuangalia makundi hayo kwa upekee zaidi  kwa kutenda haki na usawa.
Mhe. Chongolo
amefafanua kuwa ili kufikia malengo hayo kila mmoja hakuna budi
kushirikiana na kamati hiyo iliyoundwa kuweka miundombinu sawia
itakayowezesha walemavu kuishi kwa kupata haki zao na usawa pamoja na
kuepusha kunyanyapaliwa kama ilivyo kwa sasa.
 “ Nawashukuru
sana kwakunipa heshima hii ya kuzindua kamati hii ambayo inalenga
kusimamia, kushughulikia  ipasavyo kutetea haki na usawa wawatu wenye
ulemavu” amesema Mhe. Chongolo.
Mhe. Chongolo
hakusita kueleza changamoto mbalimbali zilizopo katika halmashauri ya
Kinondoni nakusema kuwa sio vijijini tu hata mijini wapo baadhi ya watu
wanao wanyanyapaa walemavu  kwakuwatenga, kuwaficha pamoja na kuwanyima
fursa yakupatiwa huduma kama watu wengine.
“ Jamii imekuwa
na taswira mbaya yakuona kwamba ulemavu ni  changamoto iliyokuwa na
madhara , na hivyo kujikita kunyanyapaa, kamati hii imepewa mamlaka,
 sasa nendeni mkajenge timu nzuri itakayoleta sura ya kubadilisha
mtazamo uliopo hivi sasa na kuleta matunda na faida kwao.
Awali taarifa ya
watu wenye ulemavu, ilieleza kuwa halmashauri inajumla ya kata 20 ambazo
zinahudumia watu hao wapatao 1239 ambapo kati yao wanaume ni 724 na
wanawake 515.
Aidha taarifa
hiyo ilieleza kuwa kati ya watu hao wakubwa ni 973 huku watoto wakiwa
266 na kwamba huduma hizo zinatolewa kwakuzingatia sera ya watu wenye
ulemavu ya mwaka 2004, sheria namba 9 ya mwaka 2010 pamoja na mikataba
mbalimbali inayohusu watu wenye ulemavu.
Ameeleza kuwa ,
halmashauri imekuwa ikiviwezesha vyama vya watu wenyeulemavu
kwakuvipatia vifaa saidizi kulingana na aina ya ulemavu sambamba na
kuwapatia misaada au kujikimu kwa walio na mazingira hatarishi.
Aidha ameeleza
kuwa , halmashauri ya Kinondoni  imekuwa ikiwaunganisha na asasi za
kiraia ili waweze kujipatia ujuzi , ajira na misaada ya kujikumu palipo
na uhitaji pamoja na kuwawezesha maadhimisho ya watu wenye ulemavu
yanayofanyika kila mwaka.