Dc chongolo atekeleza agizo la rais jpm la kusimamia kurudishwa kwa nyumba ya bibi mwenye miaka zaidi ya 80.


 Nyumba aliyokabidhiwa Bi Amina Muhenga baada ya rais Dk. Magufuli
kutoa agizo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo na
hivyo kulifanyia kazi.
Bi Amina Muhenga
aliyekaa chini akimshukuru na kumuombea mungu Rais Dk. John Magufuli
muda mchache kabla ya kukabidhiwa hati yake ya nyumba. Aliyesimama
kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni , Mhe.
Daniel Chongolo akimsalimia Bi Amina Muhenga ambaye alizurumiwa nyumba
miaka zaidi ya 30 iliyopita muda mfupi kabla ya kumkabidhi hati ya
umiliki wa nyumba. Wanaoshuhudia ni wananchi wa eneo la Mkoroshini Kata
ya Msasani.
                                                           
Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo ametekeleza agizo la Rais Dk. John Pombe
Magufuli la kusimamia kurudishwa kwa nyumba ya Bi Amina Muhenga mwenye
miaka zaidi ya 80 aliyozurumiwa kwa kipindi cha miaka zaidi ya 30
iliyopita.
Rais Dk.
Magufuli alitoa agizo hilo zaidi ya miezi miwili iliyopita alipokuwa
kwenye ibada ya jumapili katika kanisa la mtakatifu Petro ambapo Bi
Amina alimfuata na kumueleza malalamiko yake kuhusiana na nyumba yake
kuchukuliwa na mtu mwingine kinyume cha taratibu na hivyo kumsababishia
kukosa makazi maalumu ya kuishi.
Mhe. Chongolo
alieleza kuwa baada ya Rais kutoa maagizo hayo, kwakuwa ni waisaidizi
wake ,walilifanyia kazi na hivyo kufanikisha kumrudishia Bi Amina nyumba
yake pamoja na hati huku utaratibu mwingine ukiendelea kufanyika.
“Baada ya
kupokea malalamiko kutoka kwa Bibi, Mhe rais  kwakuwa sisi ni wasaidizi
wake, alituagiza kulifanyia kazi na leo hii tumehitimisha kwa kumkabidhi
hati za umiliki wa nyumba yake, na mambo mengine tunaendelea
kuyakamilisha, kuanzia sasa bibi anarudi kwenye nyumba yake.” Amessema
Mhe. Chongolo.
Aidha Mhe.
Chongolo ameonyesha masikitiko yake ya baadhi ya wananchi wanaoishi
katika Wilaya ya Kinondoni kuishi kwa ujanja ujanja na kusema kuwa
kunaidadi kubwa ya watu wanaoishi kwenye mfumo huo na hivyo kutoa onyo
la kuwataka kuacha mara moja tabia hiyo.
Amesema
imekuwa ni jambo la kawaida kwa wananchi hao kwani kila siku ofisi yake
imekuwa ikipokea malalamiko yanayohusiana na kuzurumiwa kwa nyumba zao
kwakutumia kigezo cha hukumu ya Mahakama na hivyo kuacha watu
wakiteseka.
Ameongeza
kuwa,wakitoka Mahakamani wanakuja kuwatoa watu wenye haki, sijui niseme
nini ila ukiangalia kunahali ya rushwa, ambayo imekuwa ikiwatesa sana
baadhi ya wananchi, kazi yetu sisi ni kusimamia haki,nitahakikisha haki
inasimamiwa na inatolewa kwa mwenye haki” amesema Mhe. Chongolo.
Kwa upande
wake Bi Amina amemshukuru rais Magufuli kwa kumsaidia kupata nyumba
yake, na hivyo kusema kuwa anamuombea kwa mungu aendelee kuwatumikia
wanyonge.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *