Dc chongolo awaweka ndani wakandarasi wa kampuni ya crje kwakushindwa kukamilisha mradi wa kiwanda cha kuchakata taka kwa wakati


Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe
Daniel Chongolo akiwa sambamba na wakandarasi wa kampuni ya CRJE katika
eneo la ujenzi wa kiwanda cha kuchakata taka kinachojengwa Mabwepande
alipofanya ziara ya kujionea maendeleo ya ujenzi wake.


Mafundi wakiendelea na kazi katika
ujenzi wa kiwanda cha kuchakata taka kinachojengwa Kata ya Mabwepande
katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.




Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni , Mhe. Daniel Chongolo amewashikilia wakandarasi wawili wenye
asili ya china wa Kampuni ya CRJE kwa kushindwa kukamilisha mradi wa
ujenzi wa kiwanda cha kuchakata taka kilichopo Mabwepande.


Mhe. Chongolo
amefikia uamuzi huo leo mara baada ya kampuni hiyo kushindwa kukamilisha
mradi huo kwa wakati huku Mhandisi mshauri wa Manispaa Emanuel Tilya
akisisitiza kuwa wamekuwa hawatoi ushirikiano wowote licha ya kwamba
yupo kwenye eneo la mradi.


Akizungumza
wakati wa ziara aliyoifanya leo ya kukagua miradi inayojengwa na
Halmashauri hiyo, Mhe. Chongolo amefafanua kuwa kwa muda mrefu amekuwa
akizungumza na mkandarasi huyo kuhusu kukamilisha mradi huo kwa muda
uliopangwa lakini hawakufanya hivyo.


Ameeleza kuwa
halmashauri inahitaji kiwanda hicho haraka ili kiweze kutumiwa na
wananchi ambao ndio wanufaika wa mradi huo lakini mkandarasi aliyepewa
kazi hiyo anawarudisha nyuma.


Ameeleza kuwa
halmashauri imeshawalipa fedha kwa ajili ya ujenzi huo lakini
kinachofanyika ni fedha hizo kuzipeleka kwenye miradi yao mingine jambo
ambalo limefanya hadi sasa kusuasua kwa mradi.


“ Nimekuja hapa
zaidi ya mara tatu, mara ya kwanza nilikuja nikaongea nao wakaniahidi
watakamilisha kwa muda uliopangwa, mara ya pili nilikuja hapa nikafoka
hadi nikakasirika lakini hali imeendelea hivi hivi, sasa sijawakamata
nimewashikilia hadi pale watakapoleta mpango kazi wao uliojitosheleza.“
amesema Mhe. Chongolo.


”Hatuwezi kukaa
na watu wa namna hii, tumetoa pesa nyingi,  kwa ajili ya kukamilisha
mradi huu mapema halafu wanatuchezea, ,kama wakileta leo, kesho
nitawaachia, kadiri watakavyowahi kuniletea huo mpango kazi wao ndio na
mimi nitawaachia, Askari kamata hao waweke ndani.


Askari huyo wa
kituo cha polisi Mabwepande alitii agizo hilo na kuwapakiza kwenye gari
kuelekea kituoni huku Mhe. Chongolo akiwafuata nyuma ili kuhakikisha
kuwa wamefikishwa mahali husika.


Mhe. Chongolo
alisisitiza kuwa hajaridhishwa na mwenendo wa ujenzi wa kiwanda hicho na
kuagiza wasiachiwe hadi  atakapotoa agizo ikiwa ni baada ya kutekeleza
walichoambiwa.


Awali Mhandisi
mshauri wa Manispaa,  mhandisi Tilya ,amesema kuwa walikubaliana kufanya
kazi usiku na mchana ili kukamilisha ujenzi huo kwa wakati lakini
kilichotokea ni tofauti huku mafundi wanne tu ndio waliokuwa wanafika
eneo hilo la mradi.


Alifafanua kuwa “
wakati mwingine huwa tunagombana wenyewe kwa wenyewe, kama angekuwa na
uwezo wakufanya kazi kama msambazaji wake ingekuwa sawa,  kwani anauwezo
wakubeba kiubiki mita. 150 hadi kufikia saa 8.00 mchana, inamana
tukifanya kazi usiku na mchana tunaweza kufikia kiubiki mita .300 kwa
siku.


Alifafanua kuwa
eneo la kiwanda hicho  kinaukubwa wa mita zaidi ya 4070 ambapo hadi sasa
tayari imeshafanyika kiubiki mita 491 sawa na asilimia 12 na kwamba
iliaweze kufanikisha hanabudi ndani ya mwezi mmoja kwa usiku na mchana
jambo ambalo alisema mkandarasi huyo hawezi kufanya.


Mhandisi huyo
alifika mbali zaidi nakusema kuwa “ hakuna ushirikiano ambao anapata
kutoka kwao ,  wanachoendelea kukifanya hapa ni kukudanganya mkuu. 


Imetolewa leo Novemba 19


Na Kitengo cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni.