Dc muheza awataka viongozi wa dini kuhamasisha jamii unywaji wa dawa za kutokomeza usubi na minyoo ya tumbo

 MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati akifungua kikao cha wajumbe wa kamati ya afya ya Msingi wilaya ya Muheza kulia ni Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza (DMO) Flora Kessy
 MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati akifungua kikao cha wajumbe wa kamati ya afya ya Msingi wilaya ya Muheza kulia ni Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza (DMO) Flora Kessy
 Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza (DMO) Flora Kessy akizungumza wakati wa kikao cha wajumbe wa kamati ya afya ya Msingi kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo
 Mratibu wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele wilayani Muheza Julias Mgeni akizungumza wakati wa kikao hicho


 Mratibu wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele wilayani Muheza Julias Mgeni akizungumza wakati wa kikao hicho
MRATIBU wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Mkoa wa Tanga Dkt Rehema Maggid akizungumza katrika kikao hicho
 mmoja wa washiriki kwenye kikao hicho akichangia jambo
 sehemu ya wajumbe kwenye kikao hicho


MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Mhandisi Mwanasha Tumbo amewataka viongozi wa dini wa taasisi za serikali na binafsi washirikiana kuwahamasisha jamii na wananchi wakijitokezea kwenye unywaji wa dawa za kutokomeza ugonjwa minyoo ya tumbo na usubi. 

Mhandisi Mwanasha aliyasema hayo wakati akifungua kikao cha wajumbe wa kamati ya afya ya Msingi wilaya ya Muheza ambapo alisema kwamba kumekuwa na fikra potofu kwamba dawa hizo zinazuia uzazi au kusababisha kansa lengo kutokomeza ugonjwa wa m inyoo na tumbu na usubi. 
Alisema kwa Sasa hawatoi dawa za kuzuia na kujikinga na matende kwa sababu wameweza kuudhibiti kwa asilimia kubwa ugonjwa huo huku akieleza mwengine uliokuwepo na sasa umekwisha ni mabusha kutokana na kufanya operesheni nyingi na umekwisha , 
Alitoa wito kwa jamii kama wapo wengine wenye matatizo hayo wajitokeza na kupatiwa matibabu na yaweze kwisha kabisa kwa jamii na hatimaye kuweza kuumaliza kabisa kwenye maeneo hayo. 
Alisema kipindi cha nyumba walikuwa wanasumbuliwa na ugonjwa wa matendo na usubi mara nyingi hawayapewi kipambele wanakuwa hawafuatilii tiba matokeo yake wakawa wanaambukizana. 
“Usubri upo hasa kandokandoi ya mito mtu anapata ugonjwa wa macho anaona ni ugonjwa wa kawaida lakini hivi sasa wamehakikisha wenye matende tunatoa kinga tiba kinga kama mtu anapata basi Kuhakikisha wadudu hao wanakufa”Alisema 
“Lakini takribani muda mrefu wananchi wa muheza wamekuwa wakipewa dawa ya matende na wilaya ya Muheza vipimo vimefanyika na kuonekana ugonjwa huo umekwisha na jitihada hizohizo tunazielekeza kwenye usubi “Alisema DC Mhandisi Mwanasha 
Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba hamasa hiyo kwa wananchi sasa ni kuhakikisha wanajitokeza waliokuwa na madhara na wasiokuwa nayo ili kuweza kupata kinga kwa sasa wamebakia asilimia 2. 
Hata hivyo alisema kwa upande wa wanafunzi wana sumbuliwa na minyooo wameweka mikakati wanafunzi wote wahakikisha wanakunywa dawa za kuzuia minyoo ili kuweza kudhibiti. 
“Lengo la Serikali chini ya Rais Dkt John Magufuli ni kuhakikisha wananchi wanakuwa na afya njema waweze kuendelea na shughuli za kiuchumi na kutekeleza kwa vitendo lakini pia na wanafunzi kusoma kwa bidii”Alisema Mkuu huyo wa wilaya. 
Awali akizungumza Mratibu wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele wilayani Muheza Julias Mgeni alisema kwamba wilaya hiyo walianza kutokumeza magonjwa manne ambayo ni kichocho, usubi, mabusha na matende, minyoo ya tumbo. 

Alisema kwa sasa kiwango cha maambukizi ya mabusha na matende kipo chini ya asilimia mbili hivyo haewaendelei tena kutoa dawa bali wanatoa elimu kwa walioathirika nalo ikiwemo upasuaji mabusha, matende wanatoa elimu.