Dc sabaya aumbuliwa: ni kuhusu tuhuma za wamiliki wa mabasi kuhujumu miundombinu ya reli “

Jeshi
la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro limesema hakuna hujuma wala uharibufu wa
miundombinu ya Reli katika eneo la Kijiji cha Rundugai Wilayani Hai kama
zilivyoelezwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Lengai Ole Sabaya .



January
19 mwaka huu Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya akiwa katika
Kijiji cha Rundugai akikagua ukarabati wa Reli alitoa agizo la kukamatwa
kwa wafanyabiashara wawili wa mabasi kwa tuhuma za kuunda genge la
uharifu ili kuathiri usafiri wa treni ya abiria kati ya Dar,Moshi hadi
Arusha.

Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro ,Kamishna Msaidizi wa Polisi ,Salum
Hamdun, amesema kuwa baada ya DC kutoa tuhuma hizo na kuagiza
wafanyabiashara wawili wa Mabasi ya Abiria, kujisalimisha polisi,
walitii agizo hilo na baada ya kutoa maelezo walitoka kwa dhamana.


“Uchunguzi wa awali umebaini kuwa hakuna miundombinu ya Reli
iliyoharibiwa au kuhujumiwa katika himaya hii kwa maana ya kipande cha
kutoka Moshi kuelekea Arusha, ambapo mpaka sasa kimeshakarabatiwa kwa
Kilomita 23 na kazi inaendelea” amesema RPC Kilimanjaro.