Dc samizi na kamanda magomi shughuli nzito katika bonanza la michezo shinyanga


Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Mussa Samizi amewataka wananchi
hasa wakazi wa kata ya Chibe kutoa taarifa za watu wanaohujumu Ujenzi wa Mradi
wa Reli ya kisasa (SGR) ili serikali iweze kuchukue hatua kali.

Ameyasema hayo kwenye Bonanza la Michezo lenye kampeni ya ’kataa uhalifu toa taarifa, Shinyanga bila uhalifu inawezekana’’ ambalo
limefanyika katika uwanja wa Chibe Manispaa ya Shinyanga na kuhudhuliwa na
viongozi  pamoja na mamia ya wananchi
toka maeneo  mbali mbali ndani ya Mkoa wa
Shinyanga.

Bonanza hilo limeandaliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali yakiwemo mashirika na taasisi za kifedha
ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Mussa
Samizi.

DC Samizi amesema serikali itaendelea kuchukua hatua kali kwa watu
watakao kamatwa ama kubainika kuwa wanahujumu rasilimali za serikali.

Amewataka wananchi Wilaya ya Shinyanga kushirikiana na serikali kupitia
jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga pamoja na jehi la jadi maarufu Sungusungu
kubaini wahalifu hasa wanaohujumu mradi wa reli ya kisasa (SGR) unaopita katika
kata ya Chibe, Old Shinyanga, Isaka pamoja na Luhumbo  na kwamba hali hiyo inakwamisha malengo ya
serikali.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi Pamoja na mambo mengine amewakumbusha
wazazi na walezi kuwajibika katika suala zima 
la malezi na makuzi ya watoto wao ili kudhibiti mmomonyoko wa maadili.

Amewasisitiza wazazi kulea watoto kwa kuzingatia mila, desturi na
tamaduni za Nchi huku akiwaomba wananchi kuwa mabalozi wazuri wa kukataa
vitendo vya ukatili ikiwemo ubakaji, ulawiti na ukatili mwingine wa kijinsia
unaoendelea katika Wilaya ya Shinyanga.

Amesema wapo baadhi ya wazazi na walezi wenye tabia za kutelekeza watoto
ambapo suala hilo hupelekea watoto hao kwenda mtaani kuwa omba omba na wengine
kuingia kwenye makundi mabaya ya kihalifu DC Samizi amesema serikali itachukua
hatua za kisheria kwa kuwashughulikia wazazi na walezi hao ili kukomesha tabia
hizo.

Aidha mgeni rasmi DC Samizi ametumia nafasi hiyo kulipongeza jeshi la
Polisi Mkoa wa Shinyanga pamoja na mratibu Amos John jina maarufu MC Mzungu
Mweuzi kwa kuandaa bonanza la michezo ikiwa 
lengo ni kuhamasisha jamii kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu katika
Mkoa wa Shinyanga.

Pia ameipongeza timu ya mpira wa miguu ya Radio Faraja FM pamoja na watu
wengine waliopata ushindi baada ya kushiriki kwenye bonanza hilo la michezo
katika uwanja wa Chibe Manispaa ya Shinyanga.

Amewasihi watu wote waliohudhuria bonanza hilo kuendeleza michezo pamoja
na mazoezi mbalimbali ya mwili ili kuimarisha Afya zao ambapo amesema hatua
hiyo pia itasaidia kuepukana na magonjwa yakuambukiza.

Kwa upande wake Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga Kamishna
msaidizi wa Polisi  ACP Janeth Magomi
ameelezea lengo la kampeni hiyo huku akiwataka  wananchi kutoa taarifa za uvunjifu wa Amani
unaojitokeza kwenye maeneo yao.

Kamanda Magomi naye amewaomba wananchi pamoja na viongozi mbalimbali
kushirikiana na jeshi la Polisi katika kutoa taarifa za watu wote ambao hawana
mapenzi mema na mradi wa Reli ya kisasa (SGR) unaopita kata ya Chibe, Oldi
Shinyanga, Isaka na Luhumbo.

ACP Magomi amewataka wakazi wa Mkoa wa Shinyanga kuacha kufanya matukio
mbalimbali yasiyofaa katika jamii ikiwemo mauaji yanayosababishwa na Imani za
kishirikiana, wivu wa mapenzi pamoja na migogoro ya Ardhi.

Ametumia nafasi hiyo pia kuwakumbusha watumiaji wa vyombo vya moto
wakiwemo waendesha pikipiki hasa wanaobeba abiria (Bodaboda) kuhakikisha
wanafuata sheria, kanuni na taratibu za usalama Barabarani ikiwemo kutembea na
Leseni, kuvaa element na  kutobeba watu
zaidi ya mmoja (Mishikaki)

Kamanda Magomi amewahakikishia wananchi pamoja na mgeni rasmi Mhe.
Johari Samizi kuwa Mkoa wa Shinyanga ni shwari na kwamba jeshi hilo litaendelea
kufanya doria na misako mbalimbali huku akisema wanashirikiana vizuri na
viongozi wa Dini (kamati ya Amani) Mkoa wa Shinyanga katika kutokomeza
wahalifu.

Baadhi ya wadau waliohudhuria Bonanza hilo akiwemo mwakilishi wa shirika
la Haki yangu Foundation Christa Christian wamesema wataendelea kushirikiana na
jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga katika juhudi mbalimbali za kupunguza au
kumaliza kabisa suala la uhalifu.

Mwakilishi wa shirika la Haki yangu Foundation Christa Christian ameitaka
jamii kufikia hatua ya kuondokana na dhana ya kufanya vitendo vya ukatili
vinavyohatarisha usalama wa maisha ya Binadamu.

Nao baadhi ya wananchi 
wamelipongeza jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kwa kufanya bonanza hilo
katika kata ya Chibe ambapo wameshukuru kwa elimu na huduma mbalimbali
walizozipata kupitia kampeni hiyo ya kata uhalifu toa taarifa, Shinyanga bila
uhalifu inawezekana.

Awali imefanyika michezo mbalimbali ambapo  washindi wameondoka na zawadi kwa upande wa
mchezo wa mpira wa miguu Radio Faraja Fm wameondoka na zawadi ya Mbuzi mmoja,
cheti cha kushiriki vyema kampeni hiyo ya kata uhalifu pamoja na Kombe baada ya
kuichapa Chibe Combine Fc bao 1-0 ambayo pia timu hiyo imeondoka na zawadi ya
mbuzi mmoja.

Mchezo mwingine uliofanyika ni mbio za baiskeli kwa wanawake
waliozunguka uwanja wa mpita wa miguu mara 10 mshindi wa kwanza ni Temineta
Charles, mshindi wa pili Grace Machiya,mshindi wa tatu Happiness Ramadhani,
mshindi wanne Dorcas Amosi na mshindi wa tano Elizabeth Hamis ambapo  Shirika la Haki Yangu Foundation limetoa
zawadi kwa washindi wote.

Kwa upande wa mbio za baiskeli kwa wanaume waliozunguka uwanja wa mpira
wa miguu mara 50 mshindi wa kwanza ni Kulwa, mshindi wa pili Masele Kichuya,
mshindi wa tatu Jelard Kondo, mshindi wa nne Said Kulwa, mshindi tano Wilson
Malaika, mshindi wa sita Mahona Kichuya, mshindi wa saba Shune Idasamaga,
mshindi wa nane Shija Said, mshindi wa tisa Luhende Mzuzu na mshindi wa 10
Salum Clement na kwamba zawadi  kwa
washindi wa mbio za baiskeli zimetolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa
Shinyanga ACP Janeth Magomi.

Kampeni ya kataa uhalifu toa taarifa, Shinyanga bila
uhalifu inawezekana imefanyika April 15,2023 ambayo imedhaminiwa na wadau
mbalimbali likiwemo Shirika la Haki Yangu Foundation, Miti Mirefu Dispensary,
Diwani kata ya Chibe, Jeshi la Polisi, Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe.
Patrobas Katambi, Soud Bakery, MC Mzungu Mweusi, Kamanda wa Jeshi la Polisi
Shinyanga ACP Janeth Magomi, Benki ya CRDB, CJ Palace, Tigo, SBC Tanzania
Limited, Malicha Microfinance, Juma Nkuba,TARURA, TANROADS, pamoja na
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Dkt. Jomaary Mrisho Satura.

  

Mkuu wa wilaya
ya Shinyanga Mhe. Johari Mussa Samizi akizungumza kwenye  Bonanza la Michezo lenye Kampeni ya ‘Kataa
Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana’ katika uwanja wa Chibe
Manispaa ya Shinyanga.
 

Mkuu wa wilaya
ya Shinyanga Mhe. Johari Mussa Samizi akizungumza kwenye  Bonanza la Michezo lenye Kampeni ya ‘Kataa
Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana’ katika uwanja wa Chibe
Manispaa ya Shinyanga.
 

Kamanda wa
jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza kwenye  Bonanza la Michezo lenye Kampeni ya ‘Kataa
Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana’ katika uwanja wa Chibe
Manispaa ya Shinyanga.
 

Kamanda wa
jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza kwenye  Bonanza la Michezo lenye Kampeni ya ‘Kataa
Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana’ katika uwanja wa Chibe
Manispaa ya Shinyanga.
 

Mkuu wa Dawati la Jinsia Mkoa wa Shinyanga SSP
Monica Sehere 
ambaye ni
Polisi Jamii Mkoa wa Shinyanga 
akizungumza kwenye  Bonanza la Michezo lenye Kampeni ya ‘Kataa
Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana’ katika uwanja wa Chibe
Manispaa ya Shinyanga.
 

Diwani wa kata ya Chibe John Kisandu akizungumza
kwenye  Bonanza la Michezo lenye Kampeni
ya ‘Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana’ katika uwanja
wa Chibe Manispaa ya Shinyanga.
 

Picha ya pamoja ya Timu ya mpira wa miguu kutoka Radio
Faraja FM Shinyanga kabla ya kuanza mchezo

.

Picha ya pamoja ya Timu ya mpira wa miguu kutoka Radio Faraja FM Shinyanga kabla ya kuanza mchezo

.

Picha ya pamoja ya Timu ya mpira wa miguu Chibe Combine Fc  kabla ya kuanza mchezo

Mgeni rasmi katika Bonanza hilo, Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akikagua timu za mpira wa miguu Chibe
Combane FC kabla ya kuanza mchezo.

Mgeni rasmi katika Bonanza hilo, Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akikagua timu za mpira wa miguu kutoka
Radio Faraja FM kabla ya kuanza mchezo.

Mchezo wa Timu ya mpira wa miguu kutoka Radio
Faraja FM na
Chibe Combine Fc ukiendelea katika uwanja wa Chibe Manispaa ya Shinyanga.

Goli ambalo lilifungwa kwa penati na mchezaji wa
timu ya mpira wa miguu kutoka Radio Faraja FM Shinyanga.

Mtangazaji kutoka Radio Faraja FM Bwana
Elisha Petro akitangaza mechi ya mpira wa miguu ya Radio Faraja wakicheza na
Chibe Combine FC

Jeshi la Jadi Sungusungu wakitoa burudani katika
Bonanza la Michezo katika uwanja wa chibe Manispaa ya Shinyanga kwenye kampeni
ya kata uhalifu toa taarifa, Shinyanga bila uhalifu inawezekana.

Jeshi la Jadi Sungusungu wakitoa burudani katika
Bonanza la Michezo katika uwanja wa chibe Manispaa ya Shinyanga kwenye kampeni
ya kata uhalifu toa taarifa, Shinyanga bila uhalifu inawezekana.

Jeshi la Jadi Sungusungu wakitoa burudani katika
Bonanza la Michezo katika uwanja wa chibe Manispaa ya Shinyanga kwenye kampeni
ya kata uhalifu toa taarifa, Shinyanga bila uhalifu inawezekana.

Viongozi na wadau mbalimbali wakitazama burudani
katika Bonanza la Michezo  uwanja wa chibe
Manispaa ya Shinyanga katika kampeni ya kata uhalifu toa taarifa, Shinyanga
bila uhalifu inawezekana.

Afisa Maendeleo ya jamii Mkoa wa Shinyanga BwanaTedson
Ngwale akizungumza  kwenye Bonanza la
Michezo lenye  Kampeni ya kataa Uhalifu
toa taarifa, Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana katika kata ya Chibe Manispaa
ya Shinyanga.

Baadhi ya wananchi ambao wamehudhuria Bonanza la
michezo lenye kampeni ya kataa uhalifu toa taarifa, Shinyanga bila uhalifu
inawezekana ambalo limefanyika kata ya Chibe Manispaa ya Shinyanga.

Baadhi ya wananchi ambao wamehudhuria Bonanza la
michezo lenye kampeni ya kataa uhalifu toa taarifa, Shinyanga bila uhalifu
inawezekana ambalo limefanyika kata ya Chibe Manispaa ya Shinyanga.

Wadau mbalimbali wakiwa katika Bonanza la michezo kata ya Chibe.










Mkuu wa
Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akikabidhi Kombe kwa mwakilishi wa timu ya mpira wa miguu kutoka
Radio Faraja FM kwa kuwa washindi katika mchezo wao.