Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Taknolojia Dkt Leonard Akwilapo
akizungumza wakati akifungua Mkutano wa wakuu wa shule za Sekondari na
Msingi za Makanisa yaliyo chini ya Kanisa Katoliki na Jumuiya ya
Kikristo Tanzania ambayo yanaratibiwa na Tume ya Kikristo ya Huduma za
Jamii (CSSC) iliyofanyika leo Januari 25,2021 jijini Dodoma.
Wakuu
wa Shule wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na
Taknolojia Dkt Leonard Akwilapo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa wakuu
wa shule za Sekondari na Msingi za Makanisa yaliyo chini ya Kanisa
Katoliki na Jumuiya ya Kikristo Tanzania ambayo yanaratibiwa na Tume ya
Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) iliyofanyika leo Januari 25,2021
jijini Dodoma.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) Bw.Peter
Maduki,akielezea jinsi wanavyotoa elimu katika shule zao wakati wa
ufunguzi wa Mkutano wa wakuu wa shule za Sekondari na Msingi za Makanisa
yaliyo chini ya Kanisa Katoliki na Jumuiya ya Kikristo Tanzania ambayo
yanaratibiwa na Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) iliyofanyika
leo Januari 25,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi
wa huduma za Elimu wa Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC)
Mwl.Petro Pamba,akitoa taarifa kwenye Mkutano wa wakuu wa shule za
Sekondari na Msingi za Makanisa yaliyo chini ya Kanisa Katoliki na
Jumuiya ya Kikristo Tanzania ambayo yanaratibiwa na Tume ya Kikristo ya
Huduma za Jamii (CSSC) iliyofanyika leo Januari 25,2021 jijini Dodoma.
Mwalimu
Deogratius Renatus kutoka Sekondari ya St.Galgan kutoka Arusha akitoa
neno la shukrani kwa mgeni rasmi mara baada ya kufungua Mkutano wa wakuu
wa shule za Sekondari na Msingi za Makanisa yaliyo chini ya Kanisa
Katoliki na Jumuiya ya Kikristo Tanzania ambayo yanaratibiwa na Tume ya
Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) iliyofanyika leo Januari 25,2021
jijini Dodoma.
Sehemu
ya washiriki wakifatilia Hotuba ya Mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa
Mkutano wa wakuu wa shule za sekondari na Msingi za Makanisa yaliyo
chini ya Kanisa Katoliki na Jumuiya ya Kikristo Tanzania ambayo
yanaratibiwa na Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC)
Katibu
Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Taknolojia Dkt Leonard Akwilapo akiwa
katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya kufungua Mkutano wa
wakuu wa shule za Sekondari na Msingi za Makanisa yaliyo chini ya Kanisa
Katoliki na Jumuiya ya Kikristo Tanzania ambayo yanaratibiwa na Tume ya
Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) iliyofanyika leo Januari 25,2021
jijini Dodoma.
Na Alex Sonna,Dodoma
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk.Leonard Akwilapo,
ameipongeza Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii(CSSC),kwa mchango wake
katika sekta ya elimu nchini huku akiahidi serikali kufanyia kazi maoni
yanayotolewa ikiwamo kupunguza kwa mitihani ya majaribio.
Akifungua
leo Mkutano wa mwaka cha Wakuu wa Shule za Sekondari na Msingi za
makanisa, Dk.Akwilapo, amesema suala la mitihani ya majaribio lina utata
na kudai kuwa ni mingi na wakati mwingine inaipa Wizara wakati mgumu
kuiratibu.
“Kuna
wengine wanadhani elimu inapatikana kwa kuuliza wanafunzi maswali mara
kwa mara, ili ng’ombe anenepe ni kuhakikisha amekula na si kumpima uzito
asubuhi, mchana na jioni, kitu kizuri ni kuimarisha
ufundishaji,”amesema.
Ameongeza
kuwa “Kuna dhana nyingine imeongezeka hadi kuweka kambi kufanyishwa
mitihani kila siku hadi jumamosi,kuna mambo tumekemea na si sahihi
kwamba ili mwanafunzi afaulu ni kupigwa mitihani, majaribio hatuyakatai
bali kila mara inamchosha mtoto.”
Aidha,
amesema nia ya serikali ni kutoleta mgongano na wanaendelea na
majadiliano na kutaka kuimarisha ufundishaji na si kupewa mitihani kila
siku.
Pia amezitaka shule kuzingatia maelekezo ya serikali katika kumkaririsha mwanafunzi darasa kwa kuwa suala hilo linalalamikiwa.
“Tunatambua
mchango wenu mnaoutoa nchini katika sekta ya elimu, hata hivyo baadhi
ya shule zisizo za serikali kama nyingine zipo kwenu au hazipo, ambazo
zinaenda kinyume na maelekezo ya serikali, niwakumbushe myazingatie
kukaririsha wanafunzi bila kuzingatia taratibu ni tatizo tunalokutana
nalo sana,”amesema.
Awali,
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume hiyo, Peter Maduki, amesema la mkutano huo
ni kuweka mikakati ya utoaji huduma bora ya elimu na kuangalia kero
zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi.
“Pia
tutajadili namna ya kuboresha huduma ya TEHAMA itatusaidia sana katika
kuboresha elimu na kupunguza gharama ya utoaji wa elimu na kuwapunguzia
mzigo wazazi,”amesema.
Ameomba
Wizara kuangalia namna ya kupunguza mitihani ya majaribio ambayo
imeonekana kuendelea kuibuka mbali na inayopaswa kufanyika kitaifa.
“Kunaendelea
kuibuka mitihani ya majaribio mara ya kikata, kiwilaya hali
inayosababisha mwingiliano wa mitihani na hii hata inashusha ubora wa
mitihani tunaomba umakini zaidi uwepo katika kuendesha
mitihani,”amesema.