Dk kalemani : marufuku nyumba za tembe na zilizoezekwa kwa nyasi kutowekwa umeme

NA SALVATORY NTANDU

Serikali
imesema itachukua hatua kali za kisheria kwa wakandarasi wanaotekeleza
miradi  ya  REA katika maeneo mbalimbali hapa nchini watakaobainika
kuzibagua nyumba za tembe na zilizoezekwa kwa majani kwa kukataa
kuzipatia nishati ya umeme nyumba hizo licha ya  wamiliki wake kulipia
gharama za huduma hiyo.


Kauli
hiyo imetolewa na Waziri wa Nishati Dk Medadi Kalemani kwenye ziara ya
siku mmoja ya kukagua utekelezaji wa mradi wa REA katika Halmashauri za
Ushetu na Msalala mkoani Shinyanga na  kupokea malalamiko ya wananchi
kutopatiwa huduma hiyo kwa kigezo cha nyumba zao kutokuwa na ubora.

“Akibainika
mkandarasi akifanya ubaguzi kwa wenye nyumba za tembe na nyasi ambao
wamelipia gharama za kuunganishiwa umeme serikali haita mvumilia
tutamchukulia hatua kali za kisheria”alisema Dk Kalemani.

Katika
hatua nyingine DK KALEMANI ametoa siku 30 kwa Mkandarasi Kampuni ya
ANGELIQUE INTERNATIONAL.LTD anayetekeleza mradi wa REA katika
halmashauri ya Ushetu kuhakikisha anakamilisha kuweka umeme katika
vijiji 54 kama mkataba wake unavyoelekeza.

“Kasi
yako ya ujenzi wa mradi huu hairidhishi ukishindwa kutimiza ndani ya
siku hizo nilizokupa hatua dhidi yako zitachukuliwa hebu ongeza
wafanyakazi na vifaa ili kwenda sambamba na masharti ya mkataba
wako”aliseme Dk Kalemani.

Fortunata
Maila ni mkazi wa Igunda katika Halmashauri ya Ushetu ni miongoni mwa
wanufauika na Mradi wa REA awamu ya Tatu amesema tangu huduma hiyo
imeanza kutolewa wamenufaika kwa kuanzisha miradi ya ujasiriamali kama
vile uzaji wa barafu vinyaji baridi kama vile soda na maji.

Kwa
upande wake Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha amesema kukamilika
kwa mradi wa umeme katika Halmshauri hizo utatoa fursa nyingi za
kujiajiri sambamba na kuwataka wananchi kuhakikisha wanailinda
miundombinu hiyo ili iweze kudumu kwani imetumia fedha nyingi za
serikali.