Waziri wa Nishati Dkt. Medard
Kalemani(Kulia) akizungumza na Mbunge wa Same Mashariki, Anne
Kilango(kushoto) wakati wa uzinduzi wa Mradi wa umeme wa Ujazilizi Fungu
la Pili A Ngazi ya Mkoa uliofanyika wilayani Same, Julai 29,2021.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani
akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Kalemane baada ya
kuwakabidhi kifaa cha UMETA kwa ajili ya kuunganishiwa umeme katika
shule yao wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Umeme wa Ujazilizi Fungu la
Pili A ngazi ya Mkoa uliofanyika katika kitongoji cha Mheza wilayani
Same, Julai 29,2021.
Mbunge wa Same Mashariki, Anne
Kilango,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa umeme wa Ujazilizi
Fungu la Pili A ngazi ya Mkoa uliofanyika wilayani Same, Julai 29,2021
uliozinduliwa na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani.
Baadhi ya wanafunzi na wananchi
wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (hayupo
pichani) wakati akizundua Mradi wa umeme wa Ujazilizi Fungu la Pili A
ngazi ya Mkoa uliofanyika wilayani Same, Julai 29,2021.
Waziri wa Nishati
Dkt. Medard Kalemani akiwa na Mbunge wa Same Mashariki, Anne
Kilango,wanafunzi pamoja na viongozi wa wilaya ya Same wakikata utepe
kuwasha umeme katika Kijiji cha Kifaru wakati wa ziara ya uzinduzi wa
Mradi wa umeme wa Ujazilizi Fungu la Pili ngazi ya Mkoa wa Kilimanjaro
uliofanyika wilayani Same, Julai 29,2021.
Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango
akisoma maelezo ya jiwe la msingi baada ya Waziri wa Nishati Dkt.
Medard Kalemani kuzindua Mradi wa umeme wa Ujazilizi Fungu la Pili
ngazi ya Mkoa uliofanyika wilayani Same, Julai 29,2021.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani
akipongezwa na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango mara baada ya
kuzindua Mradi wa umeme wa Ujazilizi Fungu la Pili A Ngazi ya Mkoa
Uliofanyika katika kitongoji cha Mheza, Julai 29,2021.
Waziri wa Nishati,
Mhe. Dkt. Medard Kalemani amewaagiza wakandarasi wanaojenga miundombinu
ya kusambaza umeme vijijini kupeleka umeme katika maeoneo maalum ambayo
yametengwa kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda.
Dkt. Kalemani alitoa
agizo hilo wakati akizindua Mradi wa Ujazilizi Umeme Vijijini Fungu la
Pili A ngazi ya mkoa uliofanyika Julai 29,2021 katika kijiji cha Mheza
wilaya ya Same Mkoa wa Kilimanjaro.
Aidha, amewakumbusha
viongozi wa Serikali za Mitaa katika ngazi ya kata na vijiji kutenga
maeneo maalum ya uwekezaji wa viwanda ili yaweze kupelekewa miundombinu
ya umeme wakati wa utekelezaji wa miradi ya kusambaza umeme vijijini.
“Tumieni umeme kufanya biashara muongeze thamani ya mazao ya kilimo na
mifugo kwa kuanzisha viwanda” alisisitiza.
Waziri Kalemani
amesema Mradi huo utatekelezwa kwa muda miezi 12 na Serikali imetenga
kiasi cha takribani Shilingi Bilioni 8.59 kwa ajili ya kuvifikishia
umeme vitongoji ambavyo havina umeme katika Mkoa wa Kilimanjaro katika
fedha hizo Wilaya ya Same imetengewa zaidi ya Shilingi Bilioni 3.
Kwa upande wake
Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Mhe. Anne Kilango Malecela
ameishukuru Serikali kwa kupelekewa miradi hiyo ya kusambaza umeme
vijijini na kuomba maeneo ambayo bado hayajafikishiwa umeme yapatiwe
nishati hiyo.