Dkt.kalemani amsimamisha kazi aliyesababisha umeme kukatika kwa uzembe

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,( kulia) akielezwa namna Mfumo wa Gridi ya Taifa,unavyofanya kazi.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani,( kushoto)akitoa maelezo kwa baadhi ya watendaji katika kituo
cha umeme cha umbongo, huku akiwa ameshika kifaa kilichokatika baada ya
kuungua na kusababisha kukatika kwa umeme usiku wa octoba, 03,2019.
Transifoma kubwa namba sita( T6)
inayozalisha umeme wa Megawati 120 iliyopata hitilafu baada ya kifunga
stimu(Fuse) kuungua na kukatika.
Mafundi wakiendelea na kazi ya
kufunga mtambo mkubwa mpya wa umeme wa Megawati 240, utakaoimarisha
huduma ya umeme kwa Mikoa wa Dar es salaam na Pwani.
Mmoja wa wasimamizi wa Kituo cha
Kupoza na Kusambaza  Umeme cha Ubungo akimuonyesha Waziri wa Nishati,
Dkt. Medard Kalemani, sehemu ambayo kifunga stimu( fuse)iliyoungua na
kukatika ilipokuwa imekaa.

 

 

Na Zuena Msuya, Dar es salaam,
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani, amemsimamisha kazi kwa uzembe, Mhandisi Samson Mwangulume wa
Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO) baada ya umeme kukatika kutokana na
hitilafu iliyotokea katika Kituo cha Kupoza na Kusambaza umeme cha
Ubungo, Jijini Dar es salaam.
Umeme huo ulikatika usiku wa Octoba 03, 2019 na kusababisha Mkoa wa Dar es salaam na Zanzibar kukosa huduma ya umeme kwa muda.
Aidha aliwataka watumishi 6 wa
TANESCO, wanaosimamia Mifumo ya Gridi ya Taifa kuhamia katika nyumba
zilizojengwa na Serikali katika Kituo cha Kupoza na kusambaza umeme cha
 Ubungo, hadi kufikia saa nane mchana ya Octoba 03,2019 akiwemo Mkuu wa
mfumo huo.
Dkt. Kalemani alisema hayo  baada
ya kufanya ziara ya kutaka kujua tatizo lililosababisha umeme kukatika,
pamoja na laini ya kusafirisha umeme kutoka katika Gridi ya Taifa juzi, Oktoba 1, 2019, katika sehemu ya Ubungo umbali wa kilometa 22 kuelekea
mkoani Morogoro.
Baada kutembelea kituo hicho na
kuona mfumo mzima wa kusafirisha umeme kwa njia ya Kieletroniki( SCADER)
na kupata maelezo kutoka kwa wataalam, imebainika kuwa chanzo cha
hitilafu hiyo ni uchafu katika vikombe(Broker) katika Transifoma kubwa
namba sita( T6) inayozalisha umeme wa Megawati 120 hivyo kusababisha
kifunga stimu( Fuse)kuungua na kukatika.
Dkt.Kalemani, alisema kutokea kwa
tatizo hilo ni uzembe uliofanywa na msimamizi aliyekuwa zamu siku hiyo
pia kutofanya kazi yake kwa ufanisi, pamoja na kutofanyika kwa ukaguzi
na matengenezo ya mitambo hiyo mara kwa mara.
“ Wataalamu wangu wamenambia kuwa
kuna fyuzi ilikatika, lakini nimetaka kujiridhisha, nimetembelea mfumo
wa usafirisha nimeona, nimekuja katika transifoma nimeona,sababu kubwa
waliyonieleza ni uchafu, sasa hili swala la uchafu ni uzembe uliofanywa
na aliyekuwa zamu kushindwa kubadilisha na kufanya usafi katika vikombe
hivyo, nimetoa maelekezo huyu Samsoni  aliyekuwa zamu namsimamisha kazi
kutokana na uzembe wake, atupishe watasimamia wengine,” alisema Dkt.
Kalemani.
Akizungumzia wasimamizi wa mfumo
wa gridi ya taifa kuishi katika nyumba zilizopo katika kituo cha ubungo,
Dkt.Kalemani alisema kuwa dhimuni la watumishi hao kuishi katika nyumba
hizo, ni kuweza kutatua kwa haraka na kwa wakati tatizo lolote
linaloweza kutokea katika mitambo hiyo, badala ya kuanza kutafutwa na
kutembea umbali mrefu kuja kutatua tatizo.
Vilevile kuimarisha  na kuongeza udhibiti na usimamizi katika Gridi ya Taifa.
Pia ametoa onyo kwa msimamizi wa
mfumo wa Gridi ya Taifa kutoka Ubungo hadi Kidato mkoani Morogoro,
kuhakikisha changamoto ya kukatika umeme kwa wakazi wa Kimara na maeneo
jirani halitokei tena na endapo litatokea aache kazi mwenyewe.
Dkt.Kalemani alilazimika kutoa
ovyo hilo, baada ya msimamizi huyo kusema kuwa tayari ameweza kudhibiti
tatizo lililokuwa likitokea mara kwa mara na kuleta adha kwa wakazi wa
eneo hilo.
Alisema kwa sasa umeme upo mwingi
nawa kutosha hivyo hakuna sababu ya kukatika, na hitilafu zinazotokea ni
kutokana na uzembe wa wahusika  kutosimamia mitambo vizuri na
kusababisha uharibufu .
Kuhusu kuimarisha huduma ya umeme
kwa Jijini la Dar es salaam, na Mkoa wa Pwani, Dkt. Kalemani alisema
kuwa tangu mwezi uliopita wameanza kufunga mtambo mpya mkubwa wa
megawati 240 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu.
Mtambo huo utakuwa mbadala wa
mitambo miwili ya zamani iliyoanza kufanya kazi tangu mwaka 1975, hivyo
kuimarisha huduma ya upatikanaji wa umeme Dar es salaam na Pwani kwa
kiasi kikubwa.
Vile vile amemuagiza Kaimu Mkuu
Msaidizi wa Kituo cha Ubungo pamoja na usambazaji wahakikishe
wanasimamia zoezi la kutoa mizigo yote iliyopo bandarini ili kuweza
kurahisisha ukamilishwaji wa ufungaji wa mtambo huo mpya ambao
umegharimu zaidi ya shilingi Bilioni 16.