Dkt nchimbi aja na mjali mtoto wa kike kwa maendeleo ya taifa

Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi  (mwenye nguo za kijani )
akiwapatia wanafunzi  wa Shule ya Sekondari Ikungi boksi la  taulo za
kike. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi(mwenye suti nyeusi) Edward
Mpogolo, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ikungi Justice
Kijazi

 Wanafunzi
wa shule ya Sekondari  ya Ikungi wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi  mara baada ya kupokea maboksi ya
taulo za kike kutoka kwa wadau mbalimbali.

Mkuu
wa Mkoa wa Singida  Dkt. Rehema Nchimbi (mwenye skafu) na Katibu Tawala
wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi wakijadiliana  mara baada ya
kutoka kwenye mkutano wa mafanikio  ya miaka 4 ya Rais Magufuli ambapo
Waziri wa TAMISEMI Suleimani Jaffo alipongeza jitihada za Mkoa wa
Singida kwenye utoaji wa huduma za afya.

Mkurugenzi
Mtendaji wa Wilaya ya Ikungi Justice Kijazi (mwenye suti ya Bluu) 
akiwa  pamoja na Mganga Mkuu wa Mkoa Singida, Victorina Ludovick (mwenye
sketi nyeusi)na Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Singida(mwenye suruali
nyeusi), Mwalimu Eva Simon Mosha wakicheza kuhamasisha uchangiaji wa
taulo za kike.
Na John Mapepele

Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi  ametoa onyo kali kwa wawekezaji
na wafanyabiasha wa kutengeneza na kuuza taulo za watoto wa kike 
kuacha  mara moja tabia ya kutengeneza taulo zisizo  na ubora kwa kuwa
Mkoa wake umeanzisha msako wa kiintelijensia na kistratejia wa kuzisaka
taulo zisizo na ubora  ambapo  atakayebainika sheria itachukua mkondo
wake mara moja.

Dkt
Nchimbi ameyasema haya leo wilayani Ikungi wakati wa zoezi maalum la
uzinduzi wa uchangishaji wa taulo za mtoto wa kike katika Mkoa wa
Singida lililopewa jina la “Mjali mtoto wa kike kwa maendeleo yake na Taifa lake
ambapo ametoa rai kwa wadau wote kushiriki kikamilifu katika kuwabaini
na kutoa taarifa za wafanyabiashara watakaojaribu kuuza taulo zisizo na
ubora ili kuwalinda watoto wa kike

Alisema
kutokana na mageuzi makubwa ya kiuchumi yanayofanywa na Serikali ya
Awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli nchi yetu imekuwa kwenye
mashindano ya kiuchumi duniani hivyo mikakati madhubuti ya kudhibiti
ubora unahitajika katika kipindi hiki kuliko kipindi kingine chochote.

Dkt
Nchimbi alisema vyombo vya dola, viongozi wa dini na wazazi wana
mchango mkubwa katika kumlinda mtoto wa kike kwa ustawi wa taifa letu.

“Ndiyo
maana tunasema na tunamaanisha kuwa tunataka kujua mipango ya udhibiti
wa ubora kwa watengenezaji hawa kwa kuwa majuto ni mjukuu, tusisubiri
kufika huko “ alisisitiza Dkt .Nchimbi

Aliongeza
kuwa ubora wa taulo za kike ni ubora wa maisha yao hivyo ni muhimu 
kuchukua hatua za kuangalia na kudhibiti mnyororo mzima wa uzalishaji na
usambazaji wa taulo sizizo kuwa na ubora.

Aidha
alitoa wito wa wajasiliamali kuja na andiko zuri la utengenezaji wa
taulo bora za kisasa zitakazotengenezwa kwa kutumia malighafi za hapa
nchini ambapo alisema mshindi atakayepatikana atamzawadia tuzo  ya
shilingi milioni moja.

Aliwataka
watoto wa kike kote nchini kujiamini kwa  kuumbwa wanawake na kwamba
hedhi ni kitu cha thamani kwa kuwa hedhi ni uhai ambapo alisisitiza 
elimu ya jinsia na mtoto wa kike kutambua mabadiliko ya miili yao
iendelea kutolewa ili kuwajenga watoto wa kike kujua thamani ambayo
mungu amewajalia kwa kuwaumba wakamilifu.

Aliwataka
wadau wote kuendelea kuchangia kwa kutambua thamani ya mtoto wa kike
ambapo katika  uzinduzi wa huu lengo lilikuwa ni kuchangia paketi 8000
za taulo za kike lakini zilipatikana jumla ya paketi 9089 kulingana na
fedha zilizotolewa.

Lengo
la jumla kwa mwaka 2020 katika Wilaya ya Ikungi ni kuchangia taulo
192,000 kwa watoto wote wa kike kwenye shule 36 za Sekondari,  na shule 
131 za Msingi  zenye jumla ya  watoto wa kike 16,000

Naye
KatibuTawala Mkoa wa Singida Dkt Angelina  Lutambi amesema Serikali
imeendelea kutoa kipaumbele katika huduma za afya zenye ubora na
zinazowafikia wananchi wote ili kuboresha afya zao.

Dkt.
Lutambi amesema Serikali inatambua umuhimu wa afya bora kwa wananchi
wake kwani afya bora ni raslimali muhimu kwa maendeleo. Maendeleo ya
Taifa letu la Tanzania yataletwa na wananchi wenye afya na wenye uwezo
wa kuzalisha mali.

Aliongeza
kuwa katika kuhakikisha kuwa wananchi wana afya bora, Serikali
imeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kutoa huduma za afya kwa
kuzingatia sera na miongozo iliyopo.

“Serikali
haitamfumbia macho mdau yoyote wa utoaji wa huduma ya afya ambaye
atafanya kazi   kwa mazoea bila kuzingatia  sheria na taratibu za utoaji
huduma na kwamba kuanzia sasa Serikali itakaa na kupanga  kwa pamoja
ili
kuwapatia wananchi huduma  bora wakati wote kwa wananchi wa Mkoa wa Singida na taifa kwa ujumla” amesisitiza Dkt. Lutambi

Aidha,
Waziri wa Nchi,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani
Jafo, amepongeza juhudi zinazofanywa  na Serikali ya Mkoa wa Singida
kwenye  utoaji wa huduma za afya  wakati akiwasilisha  mafanikio ya
TAMISEMI kwa kipindi cha miaka mine ya Rais Magufuli

Mkurugenzi
Mtendaji wa Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi alimshukuru Mkuu wa Mkoa
kwa wazo la kutaka Halmashauri zote katika Mkoa wa Singida kutoa elimu
ya jinsia mashuleni na kuwachangia wa watoto wa kike taulo hizo kwa kuwa
jambo lenye manufaa kwa taifa kwa kuwa ukimuelimisha mtoto  wa kike
umeelimisha taifa zima.

Alizitaja
baadhi ya changamoto zinazowakabili watoto wa kike kuwa ni pamoja na
mimba za utotoni,kubakwa,kuozeshwa katika umri mdogo na kufanyishwa
kazi  nyingi nyumbani.

Mratibu
wa program hii ya  uchangiaji wa taulo za mtoto wa kike ambaye pia ni
Afisa Maendeleo wa jamii wilaya ya Ikungi Haika Massawe alipendekeza
wazazi wahusishwe kikamilifu katika  program hii.

Alisema
vyombo vya Serikali  kama polisi na mahakama  vitende  haki katika
kushughulikia haki za mtoto wa kike aidha  wazazi wa wanafunzi wa kike
mashuleni  waelekezwe kutoa fedha  maalum kwa ajili ya kununua taulo za
watoto wao.