Dkt tulia ashiriki tamasha la kuimarisha jumuiya ya uvccm mkoani mbeya

November
2, 2019 Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson alikuwa Mgeni rasmi katika
Tamasha la kuimarisha Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM mkoa wa Mbeya
lililofanyika katika viwanja vya Sokoine ambapo kupitia taasisi yake ya
Tulia Trust ametoa michango mbalimbali kwa makundi tofauti
yalishoshiriki katika tamasha hilo.

Miongoni
mwa michango hiyo ni pamoja na kituo cha Afya cha Makongolosi Chunya
ambacho kimepata Shilingi Milion tano (Tsh 5,000,000/-), Umoja wa
Wanawake Tanzania mkoa wa Mbeya waliopewa Computer mpakato yenye thamani
ya Milion mbili (Tsh 2,000,000/-), 

Umoja
wa vijana CCM mkoa wa Mbeya waliopewa Pikipiki moja yenye thamani ya
shilingi Milion mbili na laki mbili (Tsh 2,200,000/-), Murua Group
wamepewa Milion mbili (Tsh 2,000,000/-) pamoja na Umoja wa Machifu
Igawilo waliopewa jumla ya shilingi Milion moja (Tsh 1,000,000/-) ambapo
jumla ya Shilingi Milion kumi na mbili na laki mbili zimetolewa
zimetolewa na taasisi hiyo ili kuwawezesha kuendesha shughuli zao kwa
ufanisi.
Katika
hotuba yake Dkt. Tulia amesema >>>“Kama mnavyofahamu kwamba
mimi sio Mbunge wa sehemu moja hivyo basi hata kwenye Wilaya nyingine
huko tumekwishafanya wote kazi na tutaendelea kufanya kazi kwa pamoja
ili kuimarisha chama chetu lakini kwa leo wenyeji wetu walikuwa ni Mbeya
jiji na lazima jumuiya zetu zifanye kazi vizuri na kwa ufanisi.”