Dkt. tulia awaomba wabunge kuiunga mkono hoja ya kuwa na siku ya mwanamke mwenye ulemavu

NAIBU Spika
Dk.Tulia Ackson,akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Uchumi wa Mapendekezo
ya Siku ya Mwanamke Mwenye Ulemavu nchini kilicho andaliwa na Taasisi
ya Ikupa Trust Fund kilichofanyika jijini Dodoma.



NAIBU Spika Dk.Tulia
Ackson,akisisitiza jambo wakati wa  Mkutano Mkuu wa Uchumi wa
Mapendekezo ya Siku ya Mwanamke Mwenye Ulemavu nchini kilicho andaliwa
na Taasisi ya Ikupa Trust Fund kilichofanyika jijini Dodoma.



Mshauri wa Bodi ya Ikupa Trust
Fund ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum,Mhe. Stella Ikupa wakati wa 
Mkutano Mkuu wa Uchumi wa Mapendekezo ya Siku ya Mwanamke Mwenye Ulemavu
nchini kilicho andaliwa na Taasisi ya Ikupa Trust Fund kilichofanyika
jijini Dodoma.



Mwenyekiti wa Taasisi ya Ikupa
Trust na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Amon
Mpanju,akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchumi wa Mapendekezo ya
Siku ya Mwanamke Mwenye Ulemavu nchini kilicho andaliwa na Taasisi ya
Ikupa Trust Fund kilichofanyika jijini Dodoma.



Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la
kutoa msaada wa Kisheria nchini (LSF), Lulu Ng’wanakilala,,akizungumza
wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchumi wa Mapendekezo ya Siku ya Mwanamke
Mwenye Ulemavu nchini kilicho andaliwa na Taasisi ya Ikupa Trust Fund
kilichofanyika jijini Dodoma.



Mkurugenzi Mtendaji wa
Twaweza,Aidan Eyakuze,akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchumi wa
Mapendekezo ya Siku ya Mwanamke Mwenye Ulemavu nchini kilicho andaliwa
na Taasisi ya Ikupa Trust Fund kilichofanyika jijini Dodoma.



Washiriki mbalimbali wakiwemo
wadau wa watu wenye ulemavu na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, wakifuatilia mkutano wa pamoja uliowakutanisha ambao
umeandaliwa na Mbunge wa Viti Maalum Stella Ikupa kupitia Taasisi ya
Ikupa Trust jijini Dodoma.



Mshauri wa Bodi ya Ikupa Trust
Fund ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum,Mhe. Stella Ikupa akiteta jambo na
Mbunge wa Jimbo la Mchinga (CCM) Mhe.Mama Salma Kikwete wakati wa
Mkutano Mkuu wa Uchumi wa Mapendekezo ya Siku ya Mwanamke Mwenye Ulemavu
nchini kilicho andaliwa na Taasisi ya Ikupa Trust Fund kilichofanyika
jijini Dodoma.




Na.Alex Sonna,Dodoma


WABUNGE wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameombwa kuunga mkono hoja ya kuwepo
kwa maadhimisho ya siku ya mwanamke mwenye ulemavu.


Kauli hiyo imetolewa na Naibu
Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson kwenye mkutano wa pamoja wa wadau wa
Walemavu na Wabunge ulioandaliwa na Taasisi ya Ikupa Trust jijini
Dodoma.


Akizungumza katika mkutano huo, Dk
Tulia amewaomba Wabunge hao kuiunga mkono hoja hiyo pindi itakapoletwa
bungeni na Mbunge wa Viti Maalum Stella Ikupa.


Naibu Spika Amesema uwepo wa siku
ya mwanamke mwenye ulemavu itasaidia kuongeza wigo wa kujadili
changamoto na matatizo wanayokumbana nayo wanawake wenye ulemavu nchini.


Dk Tulia amesema uwepo wa siku
hiyo utatoa nafasi kubwa ya kujadili nafasi ya mwanamke mwenye ulemavu
kwani kwa kipindi kirefu wamekua wakipata changamoto bila kuwa na sehemu
ya kuziwasilishia.


” Ni kweli Walemavu wanakabiliwa
na changamoto kubwa sana lakini wanawake wenye ulemavu changamoto zao ni
kubwa zaidi, Kuna ambapo wanafanyiwa ukatili wa kimaumbile lakini
hawawezi kujitetea, ni jukumu letu kama Wabunge kuipitisha hoja hii ili
iweze kuwepo siku ya wanawake wenye ulemavu.


Niwaombe wabunge kuhakikisha kuwa
hoja hiyo itakapoletwa bungeni iwe kwa kuletwa na Mbunge Stella Ikupa
mwenyewe au hata Mbunge mwingine basi tuiunge mkono kwa asilimia 100,
ili bunge liweze kuridhia, naamini Wabunge mmetuelewa,” Amesema Dk
Tulia.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Taasisi hiyo ya Ikupa Trust ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Katiba na Sheria, Amon Mpanju amewaomba Wabunge hao kuipitisha siku hiyo
kwa manufaa ya Watu wenye ulemavu.


“Hii hoja siyo yetu pekee yetu
hata wenzetu wa shirika la kimataifa la Un Woman pamoja na shirika la
idadi ya watu duniani UNFPA wametuunga mkono katika hili la kuwa na siku
hii rasmi,” Amesema Mpanju.


Nae Mbunge Stella Ikupa amesema
kupitia uwepo wa siku ya mwanamke mwenye ulemavu ni rahisi jamii
kubadilisha mtazamo hasi dhidi ya watu wenye ulemavu na kuitumia pia
siku hiyo kama sehemu ya kutoa Elimu kwa wananchi dhidi ya vitendo
vyenye ukatili.


” Ni ombi langu kwenu Ndugu zetu
Wabunge tutakapoileta hoja hii basi iweze kupita, tunaamini kuwa na siku
moja Maalum ya wanawake wenye ulemavu kunaweza kusaidia kupunguza
vitendo vya ukatili Kwenye jamii yetu,” Amesema Mhe. Ikupa.