MKUU wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare akizungumza wakati wa uzinduzi wa wasrha hiyo kushoto ni Kaimu meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Morogoro William Masome
Sehemu ya wanachama wa chama cha wasioona Tanzania (TLB) mkoani Morogoro.
Sehemu ya wanachama wa chama cha wasioona Tanzania (TLB) mkoani Morogoro Mkuu wa Mkoa huo ambaye hayupo pichani
wanachama wa chama cha wasioona Tanzania (TLB) mkoani Morogoro.
la Umeme Nchini TANESCO limeendesha semina maalum inayohusu masuala ya
Umeme kwa wanachama wa chama cha wasioona Tanzania (TLB) mkoani
Morogoro.
wakati wa uzinduzi wa warsha hiyo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole
Sanare amesema kuwa Tanesco imeonyesha mfano mzuri wa kuigwa kwa kutoa
elimu hiyo kwa watu wa kundi maalum katika jamii.
pia kupitia hili shirika limetoa taswira kuwa mashirika ya Umma
yanafuata muelekeo wa Raisi John Pombe Magufuli ambae ni Raisi wa
wanyonge na kwa kujali wateja wake hata wa Makundi maalum kwa kutoa
elimuYa Umeme itakayowasaidia katika maisha yao ya kila siku.
huyo wa Mkoa amewataka wasioona kutokuwa wanyonge kwakudhani kuwa
Serikali haiwatambui na kusema kuwa Serikali ipo pamoja nao na
kuwakaribisha katika ofisi za Mkoa, muda wowote watakapokua na
changamoto zozote.
Kaimu meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Morogoro
William Masome amesema Kuwa TANESCO chini ya Mkurugenzi Mtendaji Dkt.
Tito Mwinuka imetambua umuhimu wa watu wenye Ulemavu wa kutoona kupatiwa
elimu ya Umeme ili waweze kutambua fursa zitokanazo na umeme
zitakazoweza kuwainua kiuchumi lakin pia kuwafundisha jinsi ya kutumia
umeme vizuri (matumizi Bora ya umeme)ili wasilipe gharama kubwa
Kwenye kununua Umeme.
kwa upande wake Mratibu wa idara ya maendeleo, Vijana na Chipkizi toka
TLB , Bw.Kiongo Itambu ameishukuru TANESCO kwa kuwapatia elimu hiyo
Maalum ambayo itawasaidia hasa katika kujiepusha na matukio ambayo yanaweza kuathiri usalama wao.
kwani wameshajua athari za kukaa karibu na miundombinu ya umeme na
kuahidi kushirikiana na TANESCO katika kuwafichua wanaolihujumu Shirika
kwa kuiba umeme na kuharibu miundombinu ya Shirika.
Bw. Kiongo alimuhakikishia Mkuu wa mkoa kuwa wao kama watu wenye
ulemavu ni kama watu wengine, ni mara chache kusikika wasioona ikiwa na
sifa ya kuliibia shirika la umeme na watakuwa mabalozi wa kuhakikisha
Tanesco haiujumiwi ili kukuza kipato chake kwa maendeleo ya Shirika na
Taifa kwa ujumla