Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imesema vigogo wa Klabu
ya Simba akiwamo Rais wa zamani, Evans Aveva na wenzake wawili
wanaokabiliwa na tuhuma za kughushi na matumizi mabaya ya madaraka,
wataanza kujitetea Novemba 20, mwaka huu.

Kesi
hiyo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,
Thomas Simba, ambapo Wakili wa Serikali, Sylvia Mitanto, aliomba tarehe
nyingine ya kusikilizwa.

Hata hivyo, Hakimu Simba alihoji kwanini kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa wakati ilipangwa kwa kusikilizwa?
Wakili
Mitanto alidai tarehe iliyopita waliitaarifu mahakama kuwa wamekata
rufani kupinga uamuzi wa mahakama hiyo kuwaona washtakiwa hawana kesi ya
kujibu katika Mashtaka ya kutakatisha fedha, na kwamba wanaomba tarehe
nyingine kusubiri uamuzi wa rufani.

Hakimu
Simba alisema mahakama hiyo itapanga tarehe ya kusikilizwa kwa utetezi
na kama kutakuwa na masuala ya rufani waijulishe mahakama.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba alisema itaanza kusikilizwa utetezi wa washtakiwa Novemba 20, mwaka huu.
Mbali
na Aveva, washitakiwa wengine ni aliyekuwa makamu wa rais, Geofrey
Nyange maarufu Kaburu na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia
Hansppope wamekutwa na kesi ya kujibu katika mashtaka saba na kuondolewa
mashtaka mawili ya utakatishaji fedha.