Gambo awataka wakandarasi kumalizia miradi ya maji kwa wakati

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Arusha alipofanya ziara ya kutembelea Kituo cha Afya Kaloleni kujionea shughuli mbalimbali kwenye kituo hicho ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku tatu kukagua miradi ya Afya na Maji kwenye Halmashauri zote za mkoa huo hii ikiwa ni ziara yake kwenye halmashauri ya jiji la Arusha mwishoni mwaka wiki picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro na mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Arusha Dkt.Maulid Madeni na Mganga mfawidhi wa kituo hicho cha Kaloleni akipata maelezo kwenye wodi ya mama na mtoto 

Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Arusha Dkt.Madeni akitoa Maelezo mbele ya Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alipotembelea kituo cha Afya Kaloleni kukagua shughuli mbalimbali kwenye kituo hicho ikiwa ni ziara ya kutembelea sekta za Afya na maji kwenye halmashauri ya jiji la Arusha mwishoni mwaka wiki

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akitoa maelekezo kwa viongozi wa wilaya ya Arusha kujenga mtaro wa Maji ili kuondoa adhaa ya kuingia kwa maji kwenye kituo cha Afya Kaloleni mwishoni mwa wiki ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku tatu kwenye halmashauri za wilaya zote za mkoa wa Arusha picha na Ahmed Mahmoud Arusha.

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiondoka kwenye kituo cha Afya Kaloleni mara baada ya kumaliza kukagua kituo hicho picha na Ahmed Mahmoud Arusha.

Sehemu ya Tanki la Maji la Ngarbob ambalo ametaka mkandarasi kuhakikisha anamaliza ndani ya muda uliopangwa na kusema limalizwe na shughuli ziendelee mchana na usiku kuona kazi hiyo inamalizika ndani ya muda uliopangwa 

Mafundi wakiendelea na kazi kwenye Tanki la Maji la Ngarbob ili wananchi wapate huduma za maji kwenye jiji la Arusha na kuondoa adhaa ya maji huo ni utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji unaogharimu kiasi cha bilioni 520 zilizotolewa na benki ya Maendeleo ya Afrika AFDB 

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akitoa maelekezo mara baada ya kukagua Mradi wa ujenzi  wa Tanki lenye kuchukuwa ujazo wa Lita milioni 2 na nusu kwenye eneo la Ngarbob nje ya jiji la Arusha

Sehemu ya Tanki la Olmot kama kilivyokutwa na kamera ya matukio jijini Arusha mwishoni mwa wiki picha na Ahmed Mahmoud Arusha.

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira jiji la Arusha AUWSA Mhandisi Rujomba kwenye Tanki la Olmot ikiwa ni ziara yake ya kukagua miradi ya sekta ya afya na Maji kwenye Halmashauri zote za mkoa huo 

Mkuu wa mkoa wa Arusha akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa AUWSA Mhandisi Faustine Rujomba

Sehemu ya Tanki la Maji la Olmot linavyoonekana kwa ndani kama lilivyokutwa na kamera ya matukio jijini Arusha mwishoni mwa wiki picha na Ahmed Mahmoud Arusha.

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiwasili kukagua miradi ya sekta ya Afya na Maji kwenye Mradi mkubwa wa Maji unaotekelezwa na mamlakani ya maji safi na usafi wa mazingira jiji la Arusha AUWSA

Mkuu wa mkoa wa Arusha akiwa na Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Arusha Dkt.Maulid Madeni na Mkurugenzi Mtendaji wa AUWSA Mhandisi Faustine Rujomba.

Ziara ya kukagua Mradi ya Maji ikiwa ni Utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za Maji kwenye Tanki la maji eneo la Burka jijini Arusha mwishoni mwa wiki 

Tanki la Maji la Olmot ambalo linalisha maji kwenye maeneo ya Olasiti na Muriet 

Viongozi wa mamlaka ya maji safi na Usafi wa mazingira pamoja na wa halmashauri ya jiji la Arusha wakibadilishana mawazo ya kuboresha sekta ya maji ikiwa ni utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji ndani ya jiji la Arusha ambao utafanya uhaba wa maji kuwa historia 

Mkuu wa mkoa wa Arusha alipowasili kukagua Maendeleo ya Ujenzi wa Kituo cha Afya Muriet ambapo alipotoa Maelekezo ya kuhakikisha hadi Alhamisi hii shughuli za utoaji wa matibabu kwenye kituo hicho pamoja na chumba cha Upasuaji kianze kazi haraka kuwapatia huduma wananchi sanjari na Daktari wa Wazee kuanza kazi na kuondoa vifaa vilivyowekwa kwenye ofisi hiyo kuhakikisha vinaungwa 

Ukaguzi ukiendelea kwenye kituo cha afya Muriet mwishoni mwa wiki

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akingojea kufunguliwa kwa chumba cha Daktari wa Wazee ambacho kimekuwa hakifanyi kazi na kugeuka kuhifadhia vifaa vya chumba cha Upasuaji na kuitaka halmashauri ya jiji la Arusha kuhakikisha hadi Alhamisi shughuli za Upasuaji zinaanza ili wananchi wapate huduma za afya.

Baadhi ya viongozi na wananchi waliombatana na Mkuu wa mkoa wa Arusha wakijionea huduma na kutoa ya moyoni ikiwemo matibabu kutotolewa kwa saa ishirini na nne na kuishia saa kumi na mbili jioni ambapo ametoa agizo kwa mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Arusha kukaa na watendaji kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya kwa muda wote.

Sehemu ya kuoshea Maiti kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha kituo cha Afya Muriet kama kilivyokutwa na kamera ya matukio jijini Arusha mwishoni mwa wiki picha na Ahmed Mahmoud Arusha.
Ukaguzi wa Tanki la Maji eneo la Muriet lenye ujazo wa lita milioni 200 picha zote na Ahmeid Mahmoud Arusha.

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amezitaka halmashauri zote mkoa wa Arusha kuhakikisha zinafunga vifaa vya Afya kwenye hospitali na vituo vya Afya sanjari na wakandarasi wa Mradi mkubwa wa maji wanaendelea na kazi za Ujenzi wa miradi hiyo usiku na mchana kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za Maji kwenye mkoa huo kama ilivyopangwa kabla ya August.

Gambo ametoa Agizo hilo Jana ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku tatu kukagua Miradi ya maji na Afya kwenye halmashauri saba za mkoa huo ambapo amesema kuwa suala hilo halihitaji kungojewa hivyo hatua zinahitajika kuchukuliwa haraka na atakuwa anafuatilia kila mara ili wananchi wapate huduma.

Amesema kuwa msingi wa ujenzi huo ambao fedha zipo na zimeshatolewa hivyo kila moja achukuwe hatua kuhakikisha serikali inatekeleza miradi kwa wakati ili ifikapo mwezi wa nane wananchi wawe wanapata huduma za maji na Afya ilikuwaondolea adha ya ukosefu wa huduma hizo.

“Nimetembea maeneo mengi kwenye sekta ya afya nimegundua vifaa tiba ikiwemo kwenye maabara na vyumba vya Upasuaji haijafungwa natoa agizo vifungwe haraka ili wananchi wapate huduma za afya sanjari na huduma za maji mkasimamie kuhakikisha wanamaliza ndani ya muda wa mkataba na kujenga miradi hiyo kwa usiku na mchana kabla ya mwezi wa nane na ikikamilika ianze kazi mara moja”

Kwa Upande wake Mkuu wa wilaya na Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Arusha Dkt.Maulid Madeni wameahidi kusimamia maagizo yote yaliotolewa na mkuu wa mkoa ili kuona wananchi wanapata huduma hizo kwa muda uliopangwa.