Gambo wenyeviti wa mitaa vijiji tembeeni kifua mbele kwa kujiamini

Na Ahmed Mahmoud Arusha

Viongozi wa mitaa,vijiji na kata fanyenikazi kwa kujiamini bila woga kwa kuwa utaratibu wa Serikali unaanzia ngazi hiyo ili muweze kutatua na kushughulika na shida za wananchi.
Aidha Mkoa wa Arusha unaweza kudhibiti vitendo vya kiuhalifu kwa raia iwapo viongozi kuanzia ngazi ya mtaa wataweza kuwajibika kwa nafasi zao kutekeleza majukumu ya kulinda usalama wa maeneo yao kwa kufichua wahalifu na vitendo vya kihalifu.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo wakati wa kikao chake na Wenyeviti wa mitaa yote ndani ya halmshauri ya Jiji la Arusha Maafisa Tarafa na watendaji wa Kata na mitaa iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa Aicc.
Alisema kuwa Jiji la Arusha linatakiwa kuhakikisha kila mtaa unakuwa na Ofisi ya Mwenyekiti wa mtaa na kama haina ofisi iliyopangwa jukumu la kulipia ni la halmashauri na hili ni agizo la Serikali.
Amewaagiza wenyeviti hao kuhakikisha watoro na wanaowapa mimba watoto wa kike wanashulika na kero hizo na watoto waliofaulu ambao hawajenda shuleni kamateni wazazi wao dhamana iwe mtoto kwenda shule.
Alisema kila moja akitimiza majukumu yake itasaidia zoezi zima la kupambana na uhalifu kwa wao kutoa taarifa za kiuhalifu pindi wanapoona wahalifu kwenye maeneo yao jambo litakalosaidia mkoa kuwa kwenye hali ya Amani na usalama na wananchi kufanya kazi zao za kujiletea maendeleo.
“Kumekuwa na hali ya kutotoa taarifa za uhalifu hivyo toeni ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kuendelea kuuweka mkoa wetu kwenye hali ya Usalama na Amani kama ulivyo Sasa ili kila mwananchi ajiletee maendeleo bila bughudha “alisema Gambo.
Kwa Upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Jonathan Shana alisema kuwa hoja ya mafunzo kwa Polisi jamii ameikubali kwa asilimia 100 na watakapokuwa teyari tuiteni kwenye mafunzo.
Alisema kuwa swala la malipo kwa Polisi jamii ni sawa lakini itokane na makubaliano na wananchi wa eneo husika kuondoa changamoto ambazo zinaweza kuepukika na kuondoa malalamiko.
Nae Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro alisema kuwa kuhusu watoto wa mitaani kwa agizo la mkuu wa mkoa wakamatwe wawekwe ndani watahakikisha wanalishughulikia suala hilo.
Alisema kuwa wataendelea kushughulikia na kupambana na vitendo vya kiuhalifu ikiwemo suala zima la ubakaji kwa kuendeleza mapambano ya  kuondoa vitendo hivyo kwenye jamii.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *