Gekul aahidi kuimarisha ushirikiano kwa wadau wa tasnia ya habari nchini

 

Rais
Samia Suluhu Hassan akimwapisha Pauline Gekul kuwa Naibu Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo katika hafla iliyofanyika katika
Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma jana.

Waziri
wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Lugha Bashungwa
(asiye na Miwani) akizungumza na Viongozi Wakuu wa Wizara; kushoto ni
Naibu wake Mhe. Pauline Gekul, kulia ni Katibu Mkuu na Msemaji Mkuu wa
Serikali, Dkt. Hassan Abbas na wa kwanza ni Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Ally
Possi, mara baada ya hafla ya uapisho iliyofanyika katika Ikulu ya
Chamwino Jijini Dodoma jana.
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Gekul na
Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Ally Possi (katikati) na Mkurugezi wa Utawala
wa Wizara hiyo Bernard Marcelline mara baada ya hafla ya uapisho
iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma jana.
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Gekul
akizungumza na Katibu Mkuu na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan
Abbas(mwenye suti ya bluu) na Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Ally Possi, mara
baada ya hafla ya uapisho iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Jijini
Dodoma jana.

·       Bashungwa
amshukuru Mhe.Rais

 

Na John Mapepele, Dodoma

 

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,  Pauline Gekul ameahidi kuimarisha
ushirikiano  kwa wadau wa  tasnia za Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
ili kutimiza  ahadi za Ilani ya Chama cha
Mapinduzi  na  ahadi alizozitoa Mheshimiwa, Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan wakati wa Kampeni za Uchaguzi   Mkuu mwaka 2020. 

Mhe. Gekul ameyasema haya muda mfupi baada ya
kuapishwa  kuwa Naibu Waziri kwenye
tasnia hizo na Mhe. Rais kwenye Ikulu ya 
Jijini Dodoma jana ambapo amewahakikishia wadau wote nchini kuendeleza
ushirikiano  ili kuleta mapinduzi makubwa
katika Wizara hiyo kwa kushirikiana na Waziri mwenye dhamana hiyo Mhe. Innocent
Bachungwa.

“ Nitatoa ushirikiano kwa Waziri wangu lakini pia kwa
wadau wote wa tasnia hii ya Wizara yetu ili kuhakikisha michezo, utamaduni,
habari, Sanaa kila jambo liende 
kulingana na ahadi alizotoa  mama
yetu mpendwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ” amesisitiza Gekul

Amesema katika kutenda kazi hii mpya pia atazingatia
miongozo aliyoitoa Mhe. Rais kwenye hotuba yake awali ambapo alielekeza mambo mahususi
ya kuyafanyia kazi.

Akizungumzia uteuzi wa Naibu Waziri Gekul mara baada
ya kukamilisha zoezi la kuwaapisha Katibu Mkuu Kiongozi, Mawaziri na Manaibu
Mawaziri, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan
amesema. “Nimemtoa Wizara ya Mifugo, pengine anajua mambo ya mifugo mifugo,
lakini nikaona aende kwenye michezo awasaidie wanawake”

Amesema wanawake wamefanikiwa kuleta vikombe vitatu
hapa nchini na hawatajwi kama ilivyo kwa upande wa wanaume ambapo ameeleza kuwa
awali yeye ndiye alipewa kazi hiyo kwenye kipindi cha kwanza cha Awamu ya Tano
na Hayati, Rais Magufuli hivyo amempa 
Mhe. Gekul kwa matarajio makubwa.

 

 Amefafanua kuwa
wanawake wamekuwa akifanya vizuri kwenye michezo mbalimbali hivyo aende
akasimamie hilo kikamilifu

“Wanawake kwenye michezo wanafanya vizuri, hawasifiwi
lakini wanaume wakishinda tu, katia goli huku viwanja vinagawiwa” ameongeza
Mhe. Rais Samia.

Naye Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,
Mhe. Innocent Bashungwa amemshukuru Mhe. Rais kwa kuwa  na Imani nao na kuendelea kuwateua kusimamia
tasnia hizo na kumuahidi kufanya kazi kwa ushirikiano, uadilifu na ubunifu
mkubwa  ili kutimiza ahadi za Serikali
kwa wananchi wake.

“Kipekee ninamshukuru 
sana Rais wangu, Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea  kutuamini naomba kumhakikishia kuwa tutafanya
kazi  bila kuchoka  na kwa ushirikiano  mkubwa 
baina yetu sote, sisi  na wadau
wetu wote ili kukamilisha ahadi katika kipindi kifupi” ameongeza Mhe. Bashungwa