Jeshi
la Polisi mkoani Singida, limethibitisha kumkamata Mbunge wa Arusha
Mjini Godbless Lema kwa ajili ya mahojiano akituhumiwa kutoa taarifa
zisizo sahihi zenye lengo la kulichonganisha jeshi hilo na wananchi
mnamo Februari 29, 2020, wilayani Manyoni.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Singida, Sweetbert Njewike amesema mtuhumiwa Lema
amekamatwa jana jioni mjini Arusha na kisha kusafirishwa hadi Singida
mjini.
Amesema hivi karibuni Lema alipokwenda Manyoni kuhudhuria mazishi ya
dereva wa boda boda Alex Joas alitumia fursa hiyo kupotosha wananchi
kwamba Jeshi la Polisi halikuchukua hatua zozote dhidi ya matukio ya
mauaji ya wakazi 14 Wilaya ya Manyoni.
Njewike amesema Lema atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.