Habari picha : mkutano wa 28 wa baraza la wafanyakazi jijini arusha

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na
Utalii, Dkt. Allan Kijazi akizungumza na watumishi katika mkutano wa 28
wa Baraza la Wafanyakazi unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo
cha Taifa cha Utalii jijini Arusha ambapo amewataka watumishi kuzingatia
sheria, kanuni na miongozo mbalimbali ili kufikia malengo yaliyowekwa.


Katibu wa Baraza, Shaha Nampeha akizungumza na watumishi ambapo
amewataka watumishi hao kufanyakazi kwa mashikamano mahali pa kazi.

Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa
Rasilimaliwatu, Lusius Mwenda akiwasilisha mada na kutoa ufafanuzi wa
masuala mbalimbali ya kiutumishi wakati wa Mkutano wa 28 wa Baraza la
Wafanyakazi la Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Arusha.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Maliasili na Utalii, Bw. Ludovick Nduhiye akizungumza wakati wa mkutano
wa 28 wa Baraza la Wafanyakazi ambapo amewataka watumishi wa Wizara ya
Maliasili na Utalii kutekeleza maagizo yote yaliyotolewa katika mkutano
huo.

Baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara ya
Maliasili na Utalii wakifuatilia maelekezo wakati Katibu Mkuu wa Wizara
ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi akizungumza na watumishi wa
Wizara hiyo katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi unaofanyika jijini
Arusha.

Mwenyekiti wa TUGHE, Anthony K.
Tibaijuka akizungumza wakati wakati wa Mkutano wa 28 wa Baraza la
Wafanyakazi ambapo amewataka watumishi kufanya kazi kwa bidii ili kukuza
na kuendeleza sekta ya maliasili na utalii.

Baadhi ya watumishi wa Wizara ya
Maliasili na Utalii wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yakitolewa na
viongozi wa Wizara hiyo katika Baraza la Wafanyakazi la 28 linalofanyika
leo jijini Arusha.