Habari zilizotufikia hivi punde : ajali yaua askari wa jwtz wawili kigoma

Na Editha KarloASKARI
wawili wa Jeshi la wananchi(JWTZ) kikosi cha 24KJ Mkoani
Kigoma,wamefariki dunia na wengine zaidi ya kumi kujeruhiwa katika
ajali  iliyotokea leo kwenye  hifadhi ya Katavi.


Askari
hao wamepata ajali baada ya gari la jeshi  lililokuwa limebeba silaha
kupinduka wakati wakielekea kwenye oparesheni Mkoani Katavi.


Kaimu
Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma maweni Lameck
Mdengo amethibitisha kupokea majeruhi hao pamoja na maiti mbili.


“Ilikuwa
majira ya saa 8 tulipokea majeruhi 20 na wawili wakiwa wamefariki dunia
ambao tumewapatia  huduma ya kwanza,wapo waovunjika mikono na miguu pia
lakini tunafanya utaratibu kuwapa rufaa ya kwenda Muhimbili au
Bugando”,alisema.
Aliwataja waliofariki  ni Bakari juma Mohamed,Rashid Abed Mwimbe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *