Halmashauri ya manispaa ya shinyanga yapongezwa

Na Mapuli Misalaba,
Shinyanga

Baadhi ya wakazi wa Mji
wa Shinyanga wamepongeza juhudi za Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga katika
utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya
Barabara na masoko.

kwa nyakati tofauti leo
wamesema kuwa yapo mabadiliko na  hatua mbalimbali za maendeleo zinazoendelea
kufanyika ikiwemo uboreshaji wa mandhari ya Mji, ujenzi na uboreshaji wa miundombinu
ya Barabara na masoko katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.

Wananchi hao wameipongeza
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga chini ya Mkurugenzi Dkt Jomaari Satura,na
mstahiki Meya Elias Ramadhani Masumbuko kwa ubunifu na usimamizi mzuri wa
mazingira na miradi mbalimbali ambayo itawanufaisha wananchi.

Wameishauri Halmashauri
ya Manispaa kuongeza ubunifu katika uibuaji wa miradi ambapo pia wameahidi
kuendelea kuunga mkono juhudi hizo,ikiwa ni pamoja na kutunza miundo mbinu
yote.

Mwonekano wa ndani katika hatua ya ujenzi wa Soko la mitumba lililopo kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga  ambalo litawanufaisha wafanyabiashara ndogo ndogo zaidi ya mia tano.