Halmashauri ya manispaa ya shinyanga yazindua programu jumuishi ya malezi makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto (pjt mmmam)

Na Mapuli Kitina Misalaba

Wazazi,walezi
na jamii katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wamekumbushwa kuhusu
kuwajibikia jukumu la malezi,makuzi na maendeleo ya awali ya  watoto.

Hayo
yamebainishwa leo Alhamis Februari 22,2024 kwenye  hafla ya uzinduzi wa Programu Jumuishi ya
Malezi Makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto (PJT MMMAM), katika Halmashauri ya
Manispaa ya Shinyanga.

Akizindua
Progamu hiyo kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,  afisa tarafa wa tarafa ya Samuye Aron Lazzer
ametaja mambo muhimu ya msingi yanayopaswa kuzingatiwa katika kipindi cha
makuzi ya ubongo ikiwemo Lishe bora, Afya bora, maji safi na salama ya kunywa
pamoja na ulinzi na usalama wa mtoto.

“Kwa nini tuwekeze kuanzia umri wa Miaka 0 hadi nane
(8) ifahamike kwamba katika kipindi hiki hapa ndipo msingi wa maisha unachukua
nafasi kiakili kimwili kijamii na kihisia na ubongo wa mtoto huanza kukua kabla
hajazaliwa”.

Wakitoa
elimu elekezi kwenye hafla hiyo, mratibu wa elimu ya afya Mkoa wa Shinyanga Dkt.
Moses Mwita ameeleza umuhimu wa afya bora kwa watoto huku akisisitiza jamii
kuzingatia misingi bora katika makuzi ya mtoto.

Vitu vya
msingi katika makuzi ya ubongo ni lishe bora, kucheza, kupumzika maji safi na
salama ya kunywa, Afya bora, ulinzi na usalama wa mtoto uchangamshi wa awali na
vifaa vya michezo kwa watoto”.amesema Dkt. Mwita

Afisa
ustawi wa jamii Mkoa wa Shinyanga Lydia Kwesigabo pamoja na mambo mengine amewataka
 washiriki kuwajibika ipasavyo ikiwa ni
pamoja na kuendelea kutoa elimu, kuhamasisha jamii kuhusu msingi wa malezi bora
kwa  watoto ili kufikia malengo
yaliyokusudiwa.

“Ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha anafanya vikao
vya mafunzo ya ngazi kwa ngazi kuhusu MMMAM kwa wakufunzi pamoja na kufanya
vikao na mikutano ya hadhara ili kuhamasisha na kuongeza uelewa kwenye jamii
lakini pia kuwatambua na kuwapa rufaa watoto wasio na vyeti vya kuzaliwa kwenda
kwenye vituo vya usajili wa vizazi vilivyokaribu lakini pia kutoa huduma za
mkoba mara kwa mara ili kuwatambua watoto wenye changamoto za ukuaji kwenye
vituo vya kulelea watoto chini ya Miaka 5, shule za awali na madarasa ya mwanzo
ya shule za msingi”.

“Tunatakiwa kwenda kufanya mikutano ya kuhamasisha
kwa viongozi wa kijamii, viongozi wa Dini, sekta binafsi na viongozi mashuhuri
kuhusu umuhimu wa kuwekeza kwa watoto wadogo kuanzia Miaka ya awali lakini pia
kuwashirikisha wanajamii, wazazi na walezi katika kusaidia kuendeleza huduma za
malezi jumuishi kwenye vituo vya kulelea watoto wadogo chini ya Miaka mitano”.
amesema
Lydia Kwesigabo

Baadhi
ya viongozi na wataalam  walioshiriki
katika hafla ya uzinduzi wa Programu Jumuishi ya Malezi Makuzi na Maendeleo ya
awali ya mtoto PJT MMMAM wamepongeza hatua hiyo ambapo  wameahidi kuwajibikia vema  utekelezaji wa programu hiyo ili kufikia
malengo yaliyokusudiwa.

 Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Progamu ya MMMAM, kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,  afisa tarafa wa tarafa ya Samuye Aron Lazzer 

Akizindua Progamu ya PJT MMMAM kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,  afisa tarafa wa tarafa ya Samuye Aron Lazzer aliyesimama katikati, leo Alhamis Februari 22,2024.

Akizindua Progamu ya PJT MMMAM kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,  afisa tarafa wa tarafa ya Samuye Aron Lazzer aliyesimama katikati, leo Alhamis Februari 22,2024.

Akizindua
Progamu ya PJT MMMAM kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya
Shinyanga,  afisa tarafa wa tarafa ya
Samuye Aron Lazzer aliyesimama katikati, leo Alhamis Februari 22,2024.

Hafla
ya uzinduzi wa Progamu ya PJT MMMAM Halmashauri
ya Manispaa ya Shinyanga, ikiendelea leo Alhamis Februari 22,2024.

Kaimu Mganga
Mkuu Manispaa ya Shinyanga, Charles Malogi akizungumza kwenye hafla ya  uzinduzi wa PJT MMMAM katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga leo Alhamis Februari 22,2024

Hafla
ya uzinduzi wa Progamu ya PJT MMMAM Halmashauri
ya Manispaa ya Shinyanga, ikiendelea leo Alhamis Februari 22,2024.

Hafla
ya uzinduzi wa Progamu ya PJT MMMAM Halmashauri
ya Manispaa ya Shinyanga, ikiendelea leo Alhamis Februari 22,2024.

Hafla
ya uzinduzi wa Progamu ya PJT MMMAM Halmashauri
ya Manispaa ya Shinyanga, ikiendelea leo Alhamis Februari 22,2024.

Mwezeshaji
mratibu wa elimu ya afya Mkoa wa Shinyanga Dkt. Moses Mwita, akitoa elimu
elekezi kwenye hafla ya uzinduzi wa PJT MMMAM, Halmashauri ya Manispaa ya
Shinyanga leo Alhamis Februari 22,2024.

Afisa ustawi wa jamii Mkoa wa Shinyanga Bi. Lydia Kwesigabo, akitoa elimu

Mwenyekiti wa Baraza la
Ushauri la wazee Manispaa ya Shinyanga, Stephano Tano 
akitoa maoni yake kwenye hafla ya  uzinduzi wa PJT MMMAM, Halmashauri ya Manispaa
ya Shinyanga

Afisa Elimu Watu
wazima Mkoa wa Shinyanga, Dedan Rutazika akizungumza kwenye uzinduzi wa  PJT MMMAM Manispaa ya Shinyanga

Afisa Elimu ya watu wazima,
Beatrice Mbonea akizungumza kwenye hafla ya 
uzinduzi wa PJT MMMAM, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
.

Afisa lishe, Amani Mwakipesile akizungumza kwenye hafla ya 
uzinduzi wa PJT MMMAM, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
.

 Mwenyekiti umoja wa miliki wa Day Care centres Manispaa ya Shinyanga, Damary Molless akizungumza kwenye hafla ya 
uzinduzi wa PJT MMMAM, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
.

 Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu Mkoa wa Shinyanga Mohamed Ally akizungumza kwenye hafla ya  uzinduzi wa PJT MMMAM, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.

 Kaimu afisa Elimu msingi Manispaa ya Shinyanga Ally Livye akizungumza kwenye hafla ya 
uzinduzi wa PJT MMMAM, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
.

 Katibu wa BAKWATA Wilaya ya Shinyanga Ramadhan Majani akizungumza kwenye hafla ya 
uzinduzi wa PJT MMMAM, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
.

 Mwinjilisti Vian Japhece kutoka kanisa la KKKT akizungumza kwenye hafla ya 
uzinduzi wa PJT MMMAM, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
.

 Mratibu kutoka shirika la SHDEPHA+ Gwalugano Katolika akizungumza kwenye hafla ya 
uzinduzi wa PJT MMMAM, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
.

 Mratibu wa Afya Manispaa ya Shinyanga Ramadhan Hamimu akizungumza kwenye hafla ya 
uzinduzi wa PJT MMMAM, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
.