Halmashauri ya ngara kukarabati kituo cha afya rukole kilichokuwa kinatumiwa na wakimbizi

Na Ashura Jumapili,Ngara 

Halmashauri ya Wilaya ya Ngara mkoani
Kagera imetenga kiasi cha shilingi milioni 600 kwa ajili ya kujenga upya
kituo cha Afya cha Rukole kilichopo kata Kasulo kilichokuwa kinatumiwa
na Wakimbikizi kabla ya kuharibika.

Kauli hiyo  ilitolewa na mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri  ya Ngara Aidan Bahama,wakati akiongea na
waandishi wa habari wilayani humo  Oktoba 27 mwaka huu.
Bahama alisema awali kituo kilikuwa
kinatumiwa  na wakimbizi  waliokuwa wanaishi kambi ya Rukole kata ya
Kasulo kabla ya kurudi kwao.
Alisema majengo hayo yalikuwa yamejengwa kwa udongo  na nyumba chache ndiyo zilikuwa za kudumu na kutokana na majengo hayo kujengwa  kwa tope  pia  yalikuwa  yameharibika.
Alisema majengo yaliyokuwa yameharibika
katika kituo hicho ni pamoja na jengo la wagonjwa wa nje  (OPD ),chumba
cha kuhifadhia maiti ( Mochwari )na hapakuwa  na chumba cha upasuaji
(Theather).
Alieleza kuwa kiasi cha shilingi milioni
600 kimetolewa  kwa ajili ya kujenga kituo hicho upya  lengo likiwa ni
kunusuru vifo vya mama na mtoto wilayani humo.
Alisema majengo yatakayojengwa kwa sasa 
ni jengo la wagonjwa wa nje (OPD ),Chumba  cha upasuaji (Theather
),chumba cha kuhifadhia maiti (Mochwari )maabara na nyumba moja  ya
watumishi.

Alisema kituo hicho kitakapokamilika kitakuwa miongoni  mwa vituo bora ambacho kitatoa huduma zote muhimu ikiwemo upasuaji.

“Tunamshukuru mheshimiwa Rais John
Magufuli,ambaye amekuwa akituletea fedha na hizi milioni 600 ni miongoni
mwa shilingi karibia bilioni 10 ambazo zimeletwa wilayani Ngara kwa
ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo”alisema mkurugenzi
huyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Ngara Aidan Bahama
Shughuli za ujenzi wa kituo cha Afya Rukore zikiendelea

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *