Halmashauri ya wilaya ya msalala kinara ukusanyaji wa mapato ya ndani
HALMASHAURI
ya Wilaya ya Msalala imekuwa ya kwanza Kitaifa katika ukusanyaji wa
mapato kwa kukusanya asilimia hamsini na mbili (52%)  ya makisio ya
mapato ya ndani kwa kipindi cha robo ya kwanza ya  mwaka wa fedha
2019/20 huku Halmashauri ya Kyerwa ikiwa ya mwisho kwa kukusanya asilimi
tatu tu ya makisio yake.Hayo
yamebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo alipokuwa akitoa taarifa ya
ukusanyaji wa mapato ya ndani ya halmashauri kwa kipindi cha Julai –
Septemba, 2019

Alisema
Halmashauri ya Wilaya ya Msalala imefanikiwa kukusanya mara mbili ya
malengo  ya robo ya kwanza ambapo kila halmashauri inatakiwa kukusanya
si chini ya asilimia 25 ya makisio ili kukamilisha asilimia 100 kwa robo
nne za mwaka wa fedha.

Waziri
Jafo alieleza kuwa Bajeti iliyoidhinishwa ya mapato ya ndani ya
Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2019/20 ni shilingi Bilioni 765.48;
Katika kipindi cha robo ya kwanza (Julai hadi Septemba, 2019)
Halmashauri zimekusanya jumla ya shilingi bilioni 166.24 sawa na
asilimia 22 ya makisio ya mwaka.

Alifafanua
kuwa “Katika kipindi hiki Halmashauri zilipaswa kukusanya asilimia 25
ya makisio yake ya mwaka lakini halmashauri hamsini na nne tu (54) ndio
zilizofanya vizuri kwa kukusanya zaidi ya asilimia 25 ya bajeti zao na
halmashauri 121 hazikuweza kufikisha asilimia 25 ya mapato yake”.

Aidha,
Mhe. Jafo alisema kuwa katika kuzipima Halmashauri zote kwa pamoja
Halmashauri ya Jiji la Dododma imekusanya mapato mengi zaidi kuliko
Halmashauri zote kwa kukusanya shilingi Bilioni 13.10 na Halmashauri ya
Buhigwe imekuwa ya mwisho kwa kukusanya shilingi Milioni 35.15.

Pia
Mhe Jafo aliongeza kuwa katika ngazi ya Mikoa, Mkoa wa Rukwa umeongoza
kwa kukusanya wastani wa asilimia thethini na moja (31) ya makisio ya
Halmashauri za Mkoa huo huku Mkoa wa Mwisho ukiwa ni Mtwara ambao
Halmashauri zake zimekusanya wastani wa asilimi kumi na tatu (13) ya
makisio yake.

Alisema
Katika kipengele hicho cha Mikoa kwa kuzingatia wingi wa mapato Mkoa
ambao unaongoza kwa kukusanya mapato ya ndani kwa wingi ni Mkoa wa Dar
es salaam ambao umekusanya shilingi Bilioni 39.53 na Mkoa wa Mwisho
katika wingi wa ukusanyaji wa mapato ni Mkoa wa Kigoma ambao umekusanya
shilingi bilioni 2.12.

Akisoma
mchanganuo wa ukusanyaji wa mapato kwa kuzingatia aina ya Halmashauri
na vigezo mbalimbali Mhe. Jafo amesema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar
es salaam imeongoza kundi la Halmashauri za Majiji kwa kukusanya mapato
kwa asilimia 38 ya makisio yake ya mwaka huku halmashauri ya Jiji la
Dodoma ikiwa ya mwisho katika kundi hili kwa kukusanya kwa asilimia kumi
na nane (18%) ya makisio yake ya mwaka.

Mhe.
Jafo alitaja Halmashauri za Majiji zilizokusanya mapato ya ndani kwa
kigezo cha wingi (Ghafi) kuwa Jiji la Dodoma limeongoza kwa kukusanya
shilingi bilioni 13.098 na Halmashauri ya Jiji la Mbeya imekuwa ya
mwisho katika kundi hili kwa kukusanya shilingi bilioni 2.74 tu.

Halkadhalika
Jafo alitaja Manispaa iliyoongoza kundi la Halmashauri za Manispaa kwa
kigezo cha asilimia kuwa ni Manispaa ya Sumbawanga ambayo imekusanya kwa
asilimia arobaini na mbili (42) na Manispaa ya mwisho katika kigezo
hiki ni Manispaa ya Kigoma ambayo imekusanya kwa asilimia tisa tu ya
makisio yake kwa mwaka.

“Katika
kigezo cha wingi wa mapato kundi hili linaongozwa na Halmashauri ya
Manispaa ya Ilala ambayo imekusanya shilingi bilioni 13.05 huku Manispaa
ya Kigoma ikiwa ya mwisho tena kwa kukusanya kiasi kidogo cha fedha cha
shilingi milioni 235.11 alisema Jafo”.

Akifafanua
kipengele cha Halmashauri za Miji Jafo alisema kuwa Mji wa Tunduma
umeongoza kwa kukusanya kwa asilimia thethini na tisa (39%) na
Halmashauri ya Mji wa Nanyamba imekua ya mwisho kwa kukusanya asilimia
nne (4%) ya makisio ya mapato yake ya ndani kwa mwaka.

Mhe.
Jafo alisema kuwa Halmashauri ya Mji wa Geita imeendelea kuongoza kwa
wingi wa mapato katika Halmashauri za Miji kwa kukusanya shilingi
bilioni 2.34 na Halmashauri ya mwisho ni Mji wa Nanyamba ambayo
imeksuanya shilingi milioni 74.72.

Wakati
huo huo Jafo alizataja Halmashauri za Wilaya zilizofanya vizuri katika
ukusanyaji wa mapato kiasilimia kuwa ni Halmashauri ya Msalala ambayo
imekusanya kwa asilimia hamisni na mbili (52%) na Halmashauri ya Kyerwa
imekuwa ya mwisho kwa kukusanya asilimia tatu (3%) ya makisio ya mapato
ya ndani kwa mwaka.

Upande
wa wingi wa mapato Mhe. Jafo alitaja Halmashauri ya Wilaya iliyoongoza
katika kundi hili kuwa ni Halmashauri ya Chalinze ambayo imekusanya
shilingi bilioni 2.05 na ya mwisho ni Halmashauri ya Buhigwe
iliyokusanya shilingi milioni thethini na tano (35) tu.

Jafo
alisema kuwa katika matumizi ya mapato ya vyanzo vya ndani katika
taarifa hii ya robo ya kwanza haionyeshi picha halisi ya uchangiaji wa
mapato hayo katika shughuli za maendeleo kwenye sekta ya Elimu, Afya na
Maji.

“Uchambuzi
kamili wa uchangiaji wa kila halmashauri katika miradi ya maendeleo
utafanyika katika robo ya pili na mwisho wa mwaka wa fedha 2019/20
lakini kila Halmashauri ifanye jitihada kuhakikisha inachangia mapato ya
ndani kulingana na asilimia inayopaswa kuchangiwa kwa mujibu wa bajeti
zake” Alifafanua Jafo.

Aidha,
Mhe. Jafo alieleza kuwa katika kipindi cha Julai-Septemba,2019
Halmashauri zilitumia shilingi Bilioni 40.88 kati ya shilingi bilioni
340.68 zilizokasimiwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo
swan a asilimia 12.

Mhe.
Jafo alikumbushia matumizi sahihi ya mifumo ya kielektroniki ya
ukusanyaji wa mapato na mashine za kukusanyia mapato (PoSs) na mifumo ya
Kielektroniki ya kutolea taarifa.

Alimalizia 
kuwataka viongozi kuweka mikakati madhubuti ya kukusanya mapato kutoka
kwenye vyanzo vipya vinavyobuniwa na Halmashauri zao

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *