Hospitali ya kanda ya kusini kuanza kazi mwakani

Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amemtaka mkandarasi wa
ujenzi wa hospitali ya rufaa ya kanda ya kusini kukamilisha ujenzi wa
hospitali hiyo ili ianze kutoa huduma ifikapo juni 2020.
Waziri Ummy ameyasema hayo leo
wakati alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa hosputali hiyo
ambayo na shirika la Taifa la nyumba (NHC)
“Nimeridhishwa na maendeleo ya
ujenzi wa hospitali hii,ninakutaka ufanye kazi usiku na mchana ili
ikiwezekana Hospitali ianze kutoa huduma ifikapo Juni,2020″.Alisisitiza
Waziri Ummy

Katika Ziara yake Waziri huyo pia alitembelea zahanati ya
Ufukoni iliyopo Manispaa ya Mtwara na kukagua utoaji wa huduma ambapo
katika kliniki ya watoto alikutana na changamoto ya uhaba wa chanjo
hususan chanjo ya Surua na kuelekeza mkoa ufanye mawasiliano ya haraka
na Mpango wa taifa wa Chanjo ili kupatiwa chanjo hizo.
Aidha, Waziri Ummy aliwataka
wananchi waliokuwa wamefika kupata huduma kwenye zahanati hiyo wajiunge
na Bima za Afya ili waondokane na tatizo la kukosa fedha za matibabu
pindi wanapohitaji matibabu
Hata hivyo katika ziara yake
kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa ya mtwara Ligula,Waziri Ummy
ameridhishwa na hali ya upatikanaji wa dawa muhimu na hivyo kuwata
viongozi wa hospitali hiyo.kuhakikisha wanatoa.vipaumbele katika masuala
yanayojitokeza ikiwemo kuhakikisha wanatafuta ufumbuzi mapema kwa
kufuata taratibu na miongozo ya kazi zao ili kuweza kuwahudumia wananchi
kwa wakati.