Jaji mkuu ataka majaji kutoa taarifa fupi kesi zenye mvuto

Na Magreth Kinabo- Mahakama
 Jaji
Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa  Ibrahim  Hamis Juma amesema ipo haja
ya  kutoa taarifa fupi kuhusu kesi zenye mvuto katika jamii ili ziweze
kueleweka kwa umma.

Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Majaji wa  Mahakama  ya Tanzania na
Majaji wa  Mahakama ya Uingereza lililoanza Februari 3 na linatarajia
kumalizika Februari 4, mwaka huu kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu
J.K . uliopo jijini Dar es Salaam, Jaji Mkuu alisema majaji ya Uingereza
wao tayari wanafanya hivyo.

‘‘Itabidi
tubadilike sisi Majaji  huenda pale tunadhani  kesi  zenye mvuto katika
jamii, tuanze  na sisi  kutoa taarifa fupi , ikiwemo kuandika hukumu
ili ujumbe uweze kufika kwa wananchi, alisema Jaji Mkuu.

Alisema
kesi hizo zinapaswa kutolewa kwa taarifa hiyo zikiwa katika nakala
ngumu na laini sambamba  na lugha ya Kiswahili na Kiingereza.

Aidha
Jaji Mkuu akizungumzia kuhusu kongamano hilo, alisema lina lengo la
kushifrikiana na kubadilishana uzoefu kwa kuwa taratibu mbalimbali za
kimahakama baina nchi hizo mbili zinafanana.

Aliongeza kuwa kupitia ushirikiano huo, tayari Majaji 21 na Mahakimu 24 wamepatiwa mafunzo.

Hivyo
kupitia ushirikiano huo, utasaidia kuleta matokeo chanya katika
maboresho yanayoendelea kwenye Mahakama ya Tanzania na  ukiwemo Mpango
Mkakati wa Miaka Mitano wa Mahakama ya Tanzania, kuanzia mwaka 2015/16
hadi 2019/20.

Kwa
upande wake, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt.
Eliezer Feleshi alisema Mahakama inafanya kazi na nchi zote  zilizopo
katika Jumuia ya Madola  ili kuweza kuboresha utendaji kazi  na kuweza
kuwa na mifumo bora na kiwango kinachokubalika.. 

Hivyo
kongamano hilo ni fursa  litasaidia kuongeza ujuzi kwa Majaji wa
Tanzania kuweza kutoa maamuzi hasa katika kesi kubwa za wawekezaji
kutoka nje ya nchi..

Dkt.
alisema nchi inaongezeka kuwa na wawekezaji wengi wa kigeni , hata
katika mahakama zetu kuna mashauri yanayofunguliwa  na kampuni za
kigeni.