Jaji mkuu wa tanzania profesa ibrahim juma atembelea mkoa wa songwe

Mkuu
wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela akionyesha Kitabu cha
Mpango wa Miaka mitano wa maendeleo ya Miundombinu ya Mahakama ya
Tanzania ambacho amekabidhiwa mapema leo na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma.


Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa
Ibrahim Juma (mwenye tai nyekundu) akikagua ramani ya eneo ambapo
itajengwa Mahakama ya Mkoa katika kijiji cha Selewa Wilaya ya Mbozi
mapema leo alipotembelea Mkoa wa Songwe.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela akisalimiana na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma (mwenye tai nyekundu) mapema leo katika eneo la Mahakama ya Mwanzo Mlowo.
Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa
Ibrahim Juma amefanya ziara ya siku Moja Mkoani Songwe na kumkabidhi
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela Mpango wa Miaka
mitano wa maendeleo ya Miundombinu ya Mahakama ya Tanzania.

Makabidhiano
hayo yamefanyika mepama leo katika Ofisi ya Hakimu wa Mkoa wa Songwe
iliyopo Vwawa ambapo Profesa Juma amesema Mpango huo utamwezesha Brig.
Jen. Mwangela kusaidia kusukuma na kufuatilia utekelezaji wake.
Profesa
Juma amesema ziara yake imelenga kuona Changamoto ambazo Mahakama inazo
kwa Mkoa wa Songwe na kwakuwa Mkoa huu ni Mpya, wameuweka katika
mipango yao kwakuwa kila sehemu yenye changamoto imewekewa ratiba ya
utekelezaji.
“Bila
kuweka Mpango Mkakati na kupanga lini unafanya nini, utajikuta hakuna
chochote kitakacho onekana kinafanyika, kwahiyo ninakukabidhi Mpango wa
Miaka Mitano wa Maendeleo ya miundombinu ya Mahakama ya Tanzania, si kwa
hapa Mkoani tu hadi katika Wilaya za Mkoa wa Songwe.”, amesema Profesa
Juma.
Katika
ziara yake Profesa Juma ametembelea Mahakama ya Mwanzo ya Mlowo,
amekagua eneo itakapojengwa mahakama ya Mkoa katika kijiji cha Selewa
Wilayani Mbozi na kutembelea Mahakama ya Mkoa iliyopo Vwawa.
Mkuu
wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela amemshukuru Profesa
Juma kwa kutembelea Mkoa wa Songwe na ana matuamini kuwa Miundo mbinu ya
Mhakama Mkoani hapa itaboreshwa.