Jamii yataka serikali kuwatia mbaroni wazazi wanaotorosha watoto shule kwa ajili ya kazi za ndani mijin

Baadhi ya wazazi na walezi katika Kijiji cha halmashauri ya mji wa
Njombe wamesema njia pekee ya kudhibiti mimba mashuleni na tabia za
wazazi kutorosha watoto mijini ili kufanya kazi za ndani hatua ambayo
inawafanya kugeuka watumwa ni kuanzisha adhabu ya kifungo Cha miezi sita
kwa mzazi yeyote atakaebainika kuhusika na uovu huo.
 Image result for Mimba za utotoni


Rai
hiyo imetolewa mara baada ya mahafali ya darasa la Saba katika shule
msingi yenye kiwango kizuri cha cha kitaaluma Echo primary school ambapo
Paul Kivavi wamesema Njombe imekumbwa sana na janga la mimba na watoto
kukimbizwa mijiji kufanya kazi Jambo ambalo linakwamisha ndoto za watoto
na mipango ya serikali hivyo adhabu ya kifungo jela Cha miezi sita
ianze  kutolewa kwa wazazi wanaobainika kuhusika ili kudhibiti matukio
hayo .


Wakati
wazazi wakitoa msimamo huo wanafunzi ambao wapo kwenye kipindi Cha
matazamio ya matokeo ya kujiunga na kidato Cha Kwanza wamesema kwamba
licha ya baadhi ya jamii fulani kushinikiza watoto kufanya vizuri katika
mitihani na kuamua kuwatorosha mijini lakini pia wazazi wengi wamekuwa
wakizembea katika malezi yenye maadili katika kipindi na kusababisha
kukengeuka .


Awali
mgeni rasmi ambaye meneja wa crdb mkoa wa Njombe akitoa wasaha kwa
wazazi na wanafunzi ametaka wazazi kuwapa watoto urithi wa elimu na
kutoa ahadi ya kumkatia bima mwanafunzi mmoja wa darasa la pili ambaye
ameonekana kukonga nyoyo za hadhara iliyohudhuria mahafali hiyo katika
somo la sayansi .