Jeshi la polisi latolea ufafanuzi kifo cha mmiliki shule ya zamzam

Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Murroto ametolea  ufafanuzi juu ya kifo
cha ustadhi Rashid Ally Mussa (62) ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya
The Dalai Islamic Center na Mmiliki wa shule ya ZAMZAM Mkazi wa
Chang’ombe Extension kuwa alifariki kutokana na tatizo la moyo kufeli na
kushindwa kufanya kazi.

Akizungumza na waandishi wa Habari wa Mkoani hapa, Kamanda muroto
amesema kabla ya kifo chake mnamo tarehe 21,Disemba,2019 alihudhuria
mkutano wa mahusiano ya  dini mbalimbali huko Jijini Dar es salam na
kurejea Dodoma tarehe 22 Disemba,2019 kwa kutumia usafiri wa basi la
kampuni ya kimbinyiko na Baada ya kufika Dodoma alifika ofisini kwake
Mtaa wa Barabara ya Nyerere,kata ya madukani, akiwa ofisini kwake
alipatwa na tatizo la moyo kufeli hivyo alifariki kutokana na kukosa
msaada wa haraka.
Wakati huo huo Kamanda muroto amesema kutokana na safari yake hiyo
alikosa mawasiliano na ndugu zake baada ya simu yake kuzima na kwa kuwa
ndugu zake walifahamu amesafiri waliendelea kumtafuta kwa njia ya simu
bila mawasiliano.
Amesema Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio na wataalamu wa uchunguzi
wa matuko kuchunguza tukio hilo ambapo eneo la tukio lilifanyiwa
uchunguzi na upekuzi katika ofisi yake na kugundua kuwa hakukuwa na
uharifu wowote ,hakuna wizi kwani upekuzi ulifanyika na kukutwa begi
dogo lenye nguo chache za safari ,simu yake ikiwa imezima,tiketi ya
safari,pesa katika wallet shilingi laki mbili na sitini (260,000) na
vitambulisho vyake.
Katika hatua nyingine amesema mwili wa marehe ulipelekwa Hospitali ya
Rufaa ya Dodoma na kufanyiwa uchunguzi na Daktari na kuthibitisha kuwa
sababu ya kifo chake ni moyo kufeli na kushindwa kufanya kazi (Cardial
Arrest).
Hatahivyo, ametoa wito kuwa watu wasitumie taarifa za kifo hicho
kupotosha umma au kuunda taarifa zenye upotoshaji kama ambazo zinaenezwa
mitandaoni