Jeshi la polisi mkoa wa shinyanga lapongezwa kamanda magomi tuliimarisha doria sikukuu ya pasaka

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limeendelea
kuimarisha hali ya ulinzi na usalama kwa kufanya doria katika maeneo mbalimbali
hali iliyosaidia wananchi kusherehekea sikukuu ya Pasaka katika mazingira ya Amani
ya utulivu.

Kwa nyakati tofauti Misalaba Blog imezungumza na
baadhi ya wakazi wa mji wa Shinyanga ambao wamelipongeza jeshi la Polisi
kuwajibikia vyema jukumu la ulinza na usalama wa raia na mali zao katika kipindi
chote cha sikukuu ya Pasaka

Wameeleza kuwa licha cha kuwepo kwa changamoto kadhaa
zilizotokana na ukiukwaji wa matumizi sahihi ya vyombo vya usafiri lakini jeshi
la polisi liliimarisha ulinzi kupitia doria zake mbalimbali.

Mwenyeviti wa wenyeviti wa serikali za mitaa
katika Manispaa ya Shinyanga Bwana Nassor Mokhe Worioba naye  ametumia nafasi hiyo kulipongeza jeshi la
Polisi Mkoa wa Shinyanga kwa kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao
huku akiwakumbusha watumiaji wa vyombo vya moto kuzingatia sheria za usalama
barabarani.

Akizungumza na Misalaba Blog  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna
msaidizi wa Polisi Janeth Magomi amesema hali ya usalama ni shwari na kwamba
jeshi hili limeendelea kuimarisha doria katika maeneo mbalimbali ya wananchi.

ACP Magomi amewashukuru wakazi wa Mkoa wa Shinyanga
kwa kuendelea kuzingatia na kufuata sheria, kanuni  na taratibu zilizopo katika kuimarisha
usalama.

Mwenyeviti wa wenyeviti wa serikali za mitaa katika
Manispaa ya Shinyanga Bwana Nassor Mokhe Worioba aliyevaa kibarakashia upande
wa kulia akiwa na baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Shinyanga ambao wamelipongeza
jeshi la Polisi kwa kuimarisha ulinzi na usalama kipindi chote cha sikukuu ya
Pasaka