Na Mapuli Misalaba,
Shinyanga
Jeshi la Polisi Mkoa wa
Shinyanga linawashikilia watuhumiwa wanne ambao wanaosadikiwa kuhusika na mtandao
wa wakata mapanga katika maeneo mbalimbali.
Katika taarifa yake kwa
vyombo vya habari Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, kamishina
msaidizi wa Polisi Leonard Nyandahu amesema watuhumiwa hao wamekamatwa kati ya
Juni 22 hadi Julai 25 mwaka huu kupitia misako na oparesheni mbalimbali kwa
lengo la kuzuia uhalifu na kuuweka Mkoa katika hali ya utulivu.
Amesema watuhumiwa hao
wamekiri kufanya matukio ya kukata watu mapanga katika maeneo mbalimbali na
kwamba mmoja kati yao amekuwa akiwadhamini wenzake kwenda kutekeleza uhalifu
huo.
Aidha, Kaimu Kamanda
Nyandahu amesema katika kipindi hicho jeshi hilo limefanikiwa kukamata vitu na
vielelezo mbalimbali ikiwemo bunduki tano ambazo zilikuwa zinakodishwa kwa watu
wengine na makampuni ya ulinzi jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
“Tumekamata
bunduki nne aina ya rifle ambazo zilikuwa zikitumika katika makampuni ya ulinzi
na kuazimana kinyume na sheria, tumekamata risasi 73 za shotgun, maganda 13 ya
risasi za shotgun, risasi za pisto 239, pikipiki mbili, Bangi kilo mbili na
kete mbili, cappet vipande 2, waya wa fensi mita 12, mali idhaniwayo kuwa ni
mali ya mgodi wa Buzwagi, mafuta ya diseal lita 310, matairi 5 ya roli
yaliyoibiwa katika mradi wa reli SGR na vifaa vya kupigia ramli chonganishi”.amesema
Nyandahu
“Kesi
33 za makossa ya jinai zikiwa na jumla ya washitakiwa 41 ziliweza kupata
mafanikio mbalimbali mahakamani ambapo kesi moja kati ya hizo niya kujeruhi
mtuhumiwa mmoja mwenye miaka 27 mkazi wa Shuni Wilaya ya Kahama Mkoa wa
Shinyanga alihukumiwa Miaka kumi jela na akitoka alipe pesa shilingi laki moja”.amesema
Nyandahu
Jeshi la polisi Mkoa wa
Shinyanga linaendelea kutoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana katika
kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu pia kufuata sheria za Nchi kwa
kutojihusishana na vitendo hivyo.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la
Polisi Mkoa wa Shinyanga, kamishina msaidizi wa Polisi Leonard Nyandahu akitoa
taarifa yake kwa waandishi wa habari, leo Jumatano Julai 26,2023.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la
Polisi Mkoa wa Shinyanga, kamishina msaidizi wa Polisi Leonard Nyandahu akionesha
vitu mbalimbali vilivyokamatwa.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la
Polisi Mkoa wa Shinyanga, kamishina msaidizi wa Polisi Leonard Nyandahu akionesha
vitu mbalimbali vilivyokamatwa.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la
Polisi Mkoa wa Shinyanga, kamishina msaidizi wa Polisi Leonard Nyandahu akionesha
vitu mbalimbali vilivyokamatwa.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la
Polisi Mkoa wa Shinyanga, kamishina msaidizi wa Polisi Leonard Nyandahu akionesha mafuta ya Diseal yaliyokamatwa.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la
Polisi Mkoa wa Shinyanga, kamishina msaidizi wa Polisi Leonard Nyandahu akionesha mali mbalimbali zilizokamatwa.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, kamishina msaidizi wa Polisi Leonard Nyandahu akionesha mali mbalimbali zilizokamatwa.