Jeshi la polisi tanzania laendelea na mikakati ya kuimarisha ulinzi na usalama katika mradi wa sgr


Makamishna pamoja na Maafisa
waandamizi wa Jeshi la Polisi Tanzania wakipata maelezo wakati wa ziara
yao katika Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kipande cha Dar es
Salaam – Morogoro hivi karibuni Septemba 2019.
Makamishna pamoja na Maafisa
waandamizi wa Jeshi la Polisi Tanzania wakipata maelezo wakati wa ziara
yao katika Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kipande cha Dar es
Salaam – Morogoro hivi karibuni Septemba 2019.
Makamishna pamoja na Maafisa
waandamizi wa Jeshi la Polisi Tanzania wakipata maelezo wakati wa ziara
yao katika Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kipande cha Dar es
Salaam – Morogoro hivi karibuni Septemba 2019.
Makamishna pamoja na Maafisa
waandamizi wa Jeshi la Polisi Tanzania wakipata maelezo wakati wa ziara
yao katika Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kipande cha Dar es
Salaam – Morogoro hivi karibuni Septemba 2019.
Makamishna pamoja na Maafisa
waandamizi wa Jeshi la Polisi Tanzania wafanya ziara katika Mradi wa
Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kipande cha Dar es Salaam – Morogoro hivi
karibuni Septemba 2019.
 
 
Lengo la ziara hiyo ni kuona
namna ya kuimarisha ulinzi ili kuhakikisha Miradi mikubwa ya kimkakati
ukiwemo mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR unalindwa na unakuwa
salama.
 
Makamishna na Maafisa hao
walipata fursa ya kuona maendeleo ya Mradi pamoja na kazi zinazoendelea
za ujenzi wa Stesheni ya Dar es Salaam, Pugu na Soga, ujenzi wa
Madaraja, tuta, vivuko, utandikaji wa reli na baadae walitembelea
kiwanda cha Mataruma kilichopo Soga mkoani Pwani.
Ziara hiyo imefanyika baada ya
kikao kazi cha Makamishna na Maafisa waandamizi wa Jeshi la Polisi
Tanzania ambapo Kamanda wa Jeshi la Polisi Nchini – IGP Simon Sirro
aliwataka Makamishna na Maafisa hao kutembelea Miradi mikubwa ili
kuimarisha mikakati ya ulinzi.
Akizungumza na Reli na Matukio
Kamishna wa Polisi Utawala na Rasilimali Watu Kamanda Benedict
Wakulyamba amesema kuwa jukumu la jeshi la polisi ni kuhakikisha ulinzi
na usalama wa raia na mali zao pamoja na mali za serikali ikiwemo Miradi
mikubwa ya kimaendeleo 


“Miradi hii mikubwa ambayo tuna jukumu la msingi la kuhakikisha
inakuwa salama na endelevu, Wajibu wetu wa kwanza ni kuhakikisha kuwa
kuna ulinzi wa kutosha” alisema Kamishna Wakulyamba
Kwa upande wake Kamishna
Mwandamizi Msaidizi wa Madawa ya Kulevya Zanzibar Kamanda Kheriyangu
Mgeni Khamis ametoa shukurani kwa Shirika la Reli Tanzania kwa kuwapa
taarifa na maelezo ya kutosha kuhusu mradi huo na amesema kuwa lengo la
ziara hiyo ni kuona jinsi ya kuboresha ulinzi na usalama katika maeneo
ya mradi. 


“Tumekuja hapa kwenye iara hii kuona ili tutakaporudi tuweze
kujipanga kimkakati kwa ajili ya ulinzi na usalama” Kheriyangu Mgeni
Khamis Kamishna Msaidizi upande wa Madawa ya Kulevya
Naye Meneja Mradi wa Ujenzi wa
Reli ya Kisasa – SGR Dar es Salaam – Morogoro Mhandisi Machibya Masanja
kwa niaba ya Shirika la Reli Tanzania – TRC amelipongeza Jeshi la Polisi
Tanzania na ameongeza kuwa Shirika limeweka mifumo ambayo haitaruhusu
reli kuhujumiwa kwa kuwa reli ya kisasa itaungwa na kuwa moja (Continous
Welded Rail), itawekewa na kufungwa na vifungashio ambavyo si rahisi
kwa mtu kufungua na kuhujumu reli

 
“Tunalipongeza jeshi la polisi kwa kuona umuhimu wa mradi, mradi
huu si wa TRC ni wa watanzania, jeshi la polisi lina nafasi kubwa ndani
ya mradi kwa sababu wao ndio wataalam wa ulinzi, tumebadilishana mawazo
juu ya mfumo wa ulinzi na usalama tulionao katika mradi, sisi kama
wahandisi tumekidhi katika kuweka mifumo ya kuhakikisha reli
haihujumiwi” alisema Mhandisi Machibya
Shirika linaendelea kuhamasisha
taasisi, jumuiya, makampuni na wananchi kwa ujumla kutoa ushirikiano kwa
kulinda miundombinu ya reli kwa sababu miundombinu hiyo ina manufaa kwa
umma wa watanzania, hivyo jukumu la ulinzi na usalama wa Miradi na
Miundombinu ya reli ni la kila mmoja wetu.