JKIC kuitumia  Hospitali  ya Wilaya ya Namtumbo  kama kituo kidogo cha  uchunguzi na matibabu ya Moyo

Joyce Joliga Namtumbo 

Taasisi  ya Moyo JKCI inatarajia kuitumia Hospitali  ya Wilaya Namtumbo  kama kituo kidogo cha  uchunguzi na Matibabu   ya moyo ili kusaidia wananchi wenye hali ya chini mkoani Ruvuma na mikoa jirani kupata matibabu  karibu na maeneo wanayoishi na kuwapunguzia gharama za kusafiri umbali mrefu kwenda kufuata matibabu.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa jimbo la Namtumbo Vita Kawawa  wakati wa uzinduzi wa kambi ya maalumu ya uchunguzi  na matiabu ya moyo ambayo inaendeshwa na Madaktari bingwa tisa wa moyo  toka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete ambayo imeanza rasmi leo 10 hadi 13  Julai 2024.

Kawawa amesema Mkurugenzi wa Taasisi ya JKCI Dkt.Peter Kisenge ameahidi  kupeleka vifaa na wataalam ili kusaidia kutibu wananchi wenye matatizo ya moyo  pamoja na kuwapatia watumishi  mafunzo ya awali ya  kutumia vifaa  ili kutoa tiba ya awali ya utambuzi wa ugonjwa wa moyo.

Amesema,kupelekwa kwa huduma ya matibabu ya moyo  wilayani humo kutasaidia kupunguza kero ya wananchi kusafiri umbali mrefu kwenda kufata huduma ya matibabu Hospitali ya Rufaa Muhimbili , Bugando na KCMC.

“Namshukuru sana mkuu wa JKCI  kwa kutupatia   wataalam hawa, pia ameahidi kutuletea vifaa na kututafutia wafadhili na ametangaza   kwanzia sasa Hospitali  ya Namtumbo itakuwa kituo kidogo cha JKCI  ili wananchi waweze kupatiwa matibabu hapahapa na madaktari bingwa toka JKCI;”Alisema Kawawa.

Aidha amemshukuru Rais Samia Suluhu kwa kuleta huduma  ya mkoba katika wilaya  hiyo kwani itatusaidia wananchi na pia ameweza kupeleka vifaa tiba, Dawa na hata kuboresha miundombinu ya majengo

Naye Kiongozi wa Madaktari  bingwa  tisa wa moyo  Dr.Baraka Ndelwa toka  taasisi ya Moyo JKCI amesema , Wagonjwa wote watakaojitokeza watapatiwa matibabu hata kama ni usiku .

” Tunauzoefu wa wa kuhudumia wagonjwa  wasiopungua 400 na watahakikisha wanawahudumia wagonjwa wote  ambao watajitokeza.”Alisema Dkt Ndelwa.

Dr.Aaron Hyera ,amesema wataalam watawasaidia wananchi wenye uwezo mdogo kupata  uchunguzi wa afya zao na matibabu  wakiwa kwenye maeneo yao 

“Hii ni mara ya tatu kwa madaktari  bingwa kuweka kambi wilayani hapo hivyo amewataka wananchi wajitokeze kwa wingi ili kuweza kupata  matibabu.”,alisema Dkt Hyera

Mbunge wa Namtumbo Vita Kawawa akizungumza na wananchi wa jimbo lake waliojitokeza kupata huduma ya matibabu

Naye  Theodora Mhuwa mkazi wa kijiji cha Likuyuseka amesema ameteseka kwa muda mrefu na ugonjwa wa moyo  kutokana na kutokuwa kuwa na uwezo wa kupata fedha za matibabu hivyo alishakata tamaa  na kusubiri kifo  hivyo kupelekwa kwa huduma hiyo kutasaidia wananchi kupata huduma za moyo toka kwa madaktari bingwa.

Kwa upande wake Halima Shauri  mkazi wa kijiji cha   Njalamatata amesema amepitia mateso makubwa ya kusafiri  mara kwa mara kwenda Muhimbili kutibiwa  tatizo la moyo hivyo kupelekwa kwa huduma  hiyo kumerejesha matumaini mapya kwa wagonjwa wa moyo.

“Niwaombe wananchi wajitoleze  kufanyiwa uchunguzi na kutibiwa ili waweze kufahamu matatizo yanayowakabili “

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *