Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Jumla ya watoto 11 wamezaliwa katika
mkesha wa sikukuu ya Krismasi katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga na
kituo cha afya Kambarage mjini Shinyanga.
Watoto wanne wamezaliwa katika Hospitali
ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga na saba katika kituo cha afya Kambarage.
Katika maelezo yake afisa muuguzi wa
Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Experantia Misalaba amesema wanawake
watatu wamejifungua kwa njia ya kawaida na mmoja amejifungua kwa njia ya
upasuaji na kwamba wote wako salama.
Kwa upande wake muuguzi mkunga wa zamu kituo
cha afya Kambarage Judith Masalu amesema kati ya wanawake 20 wajawazito
waliolazwa katika kituo hicho saba kati yao wamejifungua kwenye mkesha wa
Krismasi.
Amesema kati ya watoto saba waliozaliwa
wanne ni watoto wa kiume na watoto wa kike ni watatu ambapo amesema mtoto mmoja
amezaliwa chini ya uzito unaotakiwa.
Baadhi ya
akina mama waliojifungua katika mkesha wa Krismasi wamepongeza huduma nzuri ambazo wameendelea kupatiwa na
madaktari na wauguzi.
Afisa muuguzi wa Hospitali ya rufaa ya
Mkoa wa Shinyanga Experantia Misalaba akizungumza leo Jumatatu Disemba 25,2023.