Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa
Shinyanga kamishna msaidizi wa Polisi Janeth Magomi, ameishauri jamii kutafuta
ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili kwa kuwashirikisha watu wa karibu, badala ya kuchukua maamuzi ya kujiua.
Ametoa wito huo wakati akizungumza na Redio Faraja kufuatia
tukio la Mwanaume mmoja anayetambulika kwa jina la Mhangwa Swila mwenye umri wa
Miaka 56 mkazi wa kitongoji cha Mwandu Kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga,kujinyonga
hadi kufa kwa kile kinachosadikiwa alikuwa na msongo wa mawazo uliosababishwa
na ugumu wa maisha
Swila
amedaiwa kujiua kwa kujinyonga na kamba ya katani kwa kile
kinachosadikiwa alikuwa na msongo wa mawazo uliochangiwa na sababu mbali mbali ikiwemo ugumu wa
maisha,pamoja na kusumbuliwa na maradhi ya macho, kiuno na mgongo.
Kamanda Magomi amewaomba wananchi
kuwashirikisha watu wa karibu katika utatuzi wa changamoto zao wakiwemo
viongozi wa dini,ndugu na jamaa, badala ya kuchukua maamuzi ya kujitoa uhai
.
Tukio la kujiua kwa Muhangwa Swila
limetokea Agosti 8, 2023 majira ya saa sita usiku ambapo marehemu alikutwa
amejinyonga juu ya mti karibu na nyumba yake katika kitongoji cha Mwandu Kata
ya Tinde wilaya ya Shinyanga.