Kamati ya bunge ya viwanda na biashara yaitaka sido kuongeza ubunifu katika huduma zinazotumia teknolojia

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Mhandisi Prof. Sylvester
Mpanduji,akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,
Biashara na Mazingira katika semina iliyofanyika leo Bungeni jijini
Dodoma



Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Mhandisi Prof. Sylvester Mpanduji
akiwaelimisha wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara
na Mazingira katika semina iliyofanyika leo Bungeni jijini Dodoma



Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Viwanda Biashara na Mazingira Mhe. Dkt Charles Kimei akitoa
maoni kuhusu uboreshaji wa huduma zinazotolewa na SIDO kwa kutumia
TEHAMA katika semina iliyotolewa na ili kuwaelimisha Kamati hiyo kuhusu
Majukumu na Mafanikio ya SIDO iliyofanyika leo Bungeni jijini Dodoma



Naibu Waziri wa Viwanda na
Biashara akizungumzia mapendekezo kuhusu uboreshaji na utoaji wa huduma
za SIDO kwa kutumia teknolojia ya Kisasa katika semina ya kuwaelimisha
wajumbe wa kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda Biashara
na Mazingira kuhusu Majukumu na Mafanikio ya SIDO iliyofanyika leo
Bungeni jijini Dodoma



Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Viwanda Biashara na Mazingira Mhe. Erick Shigongo
akitoa maelekezo kwa SIDO kuongeza juhudi na ubunifu katika utoaji wa
huduma ili kukuza viwanda na kuongeza ajira nchini katika semina ya
kuwaelimisha wajumbe kuhusu Majukumu na Mafanikio ya SIDO iliyofanyika
leo Bungeni jijini Dodoma



Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Viwanda Biashara na Mazingira Mhe. Erick Shigongo
akisisitiza jambo kwa SIDO kuongeza juhudi na ubunifu katika utoaji wa
huduma ili kukuza viwanda na kuongeza ajira nchini katika semina ya
kuwaelimisha wajumbe kuhusu Majukumu na Mafanikio ya SIDO iliyofanyika
leo Bungeni jijini Dodoma



Naibu Waziri wa Viwanda na
Biashara akijumuisha maoni na mapendekezo kuhusu uboreshaji na utoaji wa
huduma za SIDO kwa kutumia teknolojia ya Kisasa katika semina ya
kuwaelimisha wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda Biashara na
Mazingira kuhusu Majukumu na Mafanikio ya SIDO iliyofanyika leo Bungeni
jijini Dodoma



Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Viwanda Biashara na Mazingira Mhe. Cecil Mwambe akitoa maoni
kuhusu SIDO kutoa huduma bora kwa teknolojia ya kisasa katika semina
iliyotolewa na ili kuwaelimisha Kamati hiyo kuhusu Majukumu na Mafanikio
ya SIDO iliyofanyika leo Bungeni jijini Dodoma



Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Viwanda Biashara na Mazingira wakisikiliza kwa makini wasilisho
kuhusu Majukumu na Mafanikio ya SIDO katika semina iliyofanyika leo
Bungeni jijini Dodoma.






KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya
Viwanda, Biashara na Mazingira imeliagiza Shirika la kuhudumia Viwanda
Vidogo (SIDO) kuongeza juhudi na ubunifu katika utoaji wa huduma
zinazotumia teknolojia ya kisasa ili kukuza viwanda vidogo na kuongeza
ajira nchini.


Hayo, yamesemwa na Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Viwanda Biashara na Mazingira, Erick Shigongo wakati wa semina
iliyolenga kuwaelimisha wajumbe wa Kamati hiyo kuhusu utekelezaji wa
majukumu ya SIDO na mafanikio yake iliyofanyika jana katika ukumbi wa
Bunge jijini Dodoma. 

 
Shigongo
amesema SIDO inatakiwa kuongeza jitihada katika kufanya utafiti na
ubunifu katika utengenezaji wa mitambo ya kisasa na inayokidhi mahitaji
na kuafanyia kazi mawazo ya vijana wengi ambao ni wabunifu lakini hawana
mitaji ya kuendeleza ubunifu wao.
 
 Naye,
Naibu Waziri wa Viwanda Exaud Kigahe (Mb) akijumuisha maoni na
mapendekezo ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara
na Mazingira alisema Serikali inaendelea kuiwezesha SIDO kuboresha
mitambo yake kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili iweze kuzalisha
mitambo yenye ubora unaokidhi mahitaji na soko shindani la mitambo
kutoka nje ya nchi.
 
 
 Amesema SIDO
imeendelea kujenga mabanda (Industrial shades) katika kila mkoa
yanayowawezesha wajasiliamali kuanzisha viwanda katika maeneo hayo kwa
urahisi.
 
 Pia alisema SIDO
imejipanga kutanua uwigo wa utuoaji huduma inayopatikana katika mikoa
yote na sasa kuelekeza huduma hizo katika kila wilaya ili kuongeza kasi
ya uanzishaji na ukuzaji wa viwanda vidogo nchini ambavyo vitaongeza
ajira na kukuza biashara na uchumi wa nchi.
 
 
 Nao,
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda Biashara na Mazingira
wametoa maoni na mapendekezo mbalimbali yanayolenga kuboresha huduma na
bidhaa zinazotolewa na SIDO ikiwemo Matumizi ya TEHAMA, kutoa huduma
bora kwa uadilifu na weledi kwa teknolojia ya kisasa, Kuanzisha vituo
vya utafiti na ubunifu, kuongeza njia za kuwawezesha vijana wabunifu ili
kuongeza ajira nchini na kuanzisha mpango wa kutoa Tuzo kwa vijana
wabunifu.
 
 
 
Akiwaelimisha Wajumbe wa Kamati hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Mhandisi Prof. Sylvester Mpanduji
amesema SIDO inatoa huduma za kiufundi na maendeleo ya teknolojia na
viwanda hususani teknolojia za kuchakata mazao ya kimkakati kama
Korosho; Alizeti, Mchikichi na nafaka katika vituo saba vya kuzalisha
teknolojia ambavyo ni Lindi, Mbeya, Iringa, Arusha, Moshi, Shinyanga na
Kigoma.
 
 

Mkurugenzi Mkuu huyo amesema huduma nyingine inayotolewa na SIDO ni
kuendeleza ubunifu wa teknolojia kwa kutumia programu ya kiatamizi
inayowalea, kuwapa mafunzo, kuwapa nafasi ya kufanyia kazi ndani ya eneo
la SIDO bure na kuwaunganisha na taasisi za kifedha wajasiliamali
wenye ubunifu wa teknolojia na mawazo ya bidhaa mpya kwa kipindi cha
miaka mitatu . 
 
Programu hii huendeshwa katika vituo vinne (Mwanza, Dar es Salaam, Mtwara na Iringa).

Amesema kuwa SIDO inashirikiana na TBS, TMDA, TRA na GPSA katika kutoa mafunzo kwa wajasiliamali katika ofisi za mikoa. 
 
Mafunzo
yanayotolewa ni mafunzo ya ujasiliamali na mbinu za biashara, Mafunzo
ya kiufundi na teknolojia na Mafunzo ya uhifadhi na usindikaji vyakula
pamoja na kuwasaidia wajasiliamali hao kupata nembo za ubora kutoka TBS.


 
 
Amesema SIDO hutoa huduma za
masoko kwa kuwashirikisha Wajasiriamali katika maonesho mbalimbali ya
bidhaa na huduma yanayoandaliwa na Serikali kupitia SIDO au taasisi
nyingine hapa nchini na nje ya nchi yakiwemo maonyesho ya kikanda na
maonesho makubwa ya kitaifa.
  
 Akiongelea
huduma za kifedha zinazotolewa na SIDO , amesema mikopo hutolewa kwa
wajasiliamali wenye viwanda vidogo kupitia mfuko wa “National
Entrepreneurship Development Fund” (NEDF), Mfuko wa dhamana (CGS) na
SANVN Viwanda Scheme ulioanzishwa kwa ushikiano wa SIDO, NSSF, VETA.
ABL, na NEEC.
 
 SIDO inashirikiana na CRDB Bank kutoa mikopo kwa viwanda vinavyochakata mazao.

Aidha akitaja mafanikio ya SIDO kati ya mwaka 2016/17 – 2019/20,
Mkurugenzi huyo amesema SIDO imefanikiwa kuanzisha Viwanda Vidogo sana
4,410, Viwanda vidogo 3,406 na Viwanda vya Kati 460. 

 
Pia
ametaja baadhi ya viwanda vikubwa vilivyoanzia SIDO kuwa ni pamoja na
Dabaga kilichopo mkoani Iringa, Mwanza Quality Wine kilichopo Mwanza,
Tausi Coffee kilichopo Shinyanga na Mart Super Brand kilichopo Manyara.

 

 
Shirika la kuhudumia Viwanda
Vidogo (SIDO) lilianzishwa kwa sheria namba 28 ya Bunge ya mwaka 1973
kwa lengo la Kushawishi, Kuhamasisha na Kusimamia uanzishwaji wa Viwanda
Vidogo nchini, Kuongeza thamani ya raslimali zilizoko nchini, Kuwezesha
kutengeneza bidhaa za kutosheleza mahitaji ya wananchi, Kuendeleza na
kutumia teknolojia rahisi inayopatikana nchini, Kutoa kipaumbele kwa
miradi ya uzalishaji inayotumia zaidi nguvukazi na Kutoa huduma kwa
viwanda vidogo nchini.